
Baadhi ya wachezaji wa Bongo Fleva wakiwa mazoezini.









TIMU za mpira wa miguu za wasanii wa
muziki, Bongo Fleva, na wacheza sinema, Bongo Movie, jana zilizidi
kutoleana vitisho kwenye mazoezi yaliyozikutanisha katika Viwanja vya
Leaders Club Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Timu ya
Bongo Movie, Jacob Steven ‘JB’, alisikika akisema kuwa hakuna mechi
itakuwa chungu kwa Bongo Fleva kama ya Tamasha la Matumaini
itakayofanyika Jumamosi hii, ambapo wanatarajia kuwapakiza mvua ya
magoli.
Nao Bongo Fleva, kupitia mchezaji wao Kala Pina, walisema
mazoezi wanayoyapata kutoka kwa kocha wao, Seleman Matola, wanawaomba
Bongo Movie wajitoe mapema mechi hiyo kwani moto wake utakuwa mkali
isivyo kawaida.
(Habari/Picha: Musa Mateja/GPL)
No comments:
Post a Comment