
Na Mwandishi wetu, DODOMA
MBUNGE
wa Viti Maalumu, Catherine Magige, amewalilia vijana kwa kuitaka
serikali kuwajiri wanaohitimu vyuo vikuu kwenda kutumikia mahakama
mbalimbali nchini badala ya kuwaacha wakihangaika mitaani.
Akichangia
katika Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Katiba na Sheria,
bungeni Dodoma, jana, Catherine alieleza kwamba vijana wengi wanaohitimu
vyuo vikuu kutoka fani ya sheria wamekuwa wakihangaika mitaani na
matokeo yake wengine kujiingiza kwenye mambo yasiyofaa.
Alisema
ugumu wa maisha wanaokumbana nao baada ya masomo unawafanya baadhi yao
kushindwa kumudu gharama za maisha na matokeo yake kujiingiza kukata
tama kimaisha.
Hivyo,
aliitaka serikali kuweka mpango ambao utakuwa unawajiri moja kwa moja
kutokana na kuonekana uhaba mkubwa wa watumishi wa mahakama, hali
itakayosaidia wengi wao kupata ajira kuliko ilivyo sasa.
“Ni
muhimu serikali kulitazama hili ili kuwasaidia vijana ambao wanajituma
kusoma kwa bidii lakini wanapohitimu masomo yao huishia kuzurura mitaani
wakitafuta ajira bila afanikio,”alieleza.
Aidha,
aliitaka serikali kuhakikisha inapunguza msongamano wa wafungwa
magerezani kwa kuharakisha kesi kuliko ilivyo sasa ambapo kuna mlundikao
mkubwa wa keshi katika mahakama nchini.
“Kuwekwe
utaratibu maalumu wa kushughulikia kesi hizo ili kupunguza mlundikano
wa kesi mahakamani, maana watu wanakaa kwa muda mrefu sana magarezani
bila kutendewa haki,”alisema.
Aidha,
aliwataka wabunge kuacha kuingilia mhimili wa mahakama kwa kuujadili
bungeni, kwani kufanyua hivyo ni kuvuka mpika ya bunge na matokeo yake
kuingilia mhimili mwingine wa dola.
“Lazima
tuheshimu mihimili mingine, vinginevyo tunawezakujikuta tukifanya mambo
ambayo hayahusiani na kazi za bunge , kitu ambacho kitaleta picha mbaya
ya bunge kuingilia mihimili mingine,”alieleza.
Pia,
aliwataka vijana kujitokeza kwa wingi katika kutoa maoni ya mchakato wa
katiba, kwani hiyo ndiyo fursa pekee kwa vijana kutambulika katika
katiba hiyo kuliko ilivyo sasa.
Alisema
kwamba kushindwa kwa vijana kutoa maoni yao katika mchakato huo ni
kupoteza fursa adhimu ambayo haitapatikana tena kwa miaka mingi ijayo,
hivyo kuwaomba kushiriki kwa wingi katika mchakato huo wa kutoa maoni.
No comments:
Post a Comment