EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Saturday, July 14, 2012

Dk Slaa ajibu hoja ya kupinga ndoa yake



Dk. Slaa akiwa na Rose Kamili 

KATIBU Mkuu wa Chadema, Dk Wilibrod Slaa, amewasilisha hoja za awali dhidi ya utaratibu wa ufunguaji wa kesi ya kupinga ndoa aliyopanga kufunga na mchumba wake wa siku nyingi, Josephine Mushumbusi.

Dk Slaa na Josephine wamepanga kufunga ndoa Julai 21 wilayani Karatu mkoani Arusha lakini juzi ilipingwa katika Mahakama Kuu ya Tanzania na mkewe, Rose Kamili.

Hoja ya Dk Slaa iliwasilishwa jana katika Mahakama Kuu ya Tanzania na wakili wake, Mutakyamirwa Philemon. Dk Slaa katika hoja hiyo, anadai kuwa suala la ndoa halikupaswa kuwasilishwa mahakamani kama la madai, bali kwa kutumia hati ya kuitwa mahakamani ikiambatanishwa na kiapo cha mdai.

Kama Kamili anayewakilishwa na wakili Joseph Tadayo atakuwa na hoja yoyote dhidi ya hoja ya Dk Slaa, atapaswa kuiwasilisha mahakamani hapo Agosti 7. Jaji Lawrence Kaduri wa Mahakama Kuu ya Tanzania aliahirisha kesi hiyo hadi Agosti 14 itakapokuja kusikilizwa.

Kamili katika kesi aliyofungua dhidi ya Dk Slaa anapinga kufungwa kwa ndoa hiyo, na pia anadai fidia ya Sh milioni 550 kwa gharama ya malezi ya familia na usumbufu aliopata kwa kutelekezwa na mumewe. Kesi hiyo ilifunguliwa na Tadayo na kusajiliwa kwa namba 5 ya mwaka huu.

Kwa mujibu wa hati ya madai iliyowasilishwa mahakamani, mdaiwa wa kwanza ni Dk. Slaa na wa pili ni Josephine. Kamili anadai kuwa yeye na Dk Slaa ni wanandoa na Josephine ndiye alisababisha Dk. Slaa atelekeze familia.

Kamili anadai yeye na Dk Slaa walifunga ndoa mwaka 1985 na Juni 18, 1987 wakajaaliwa mtoto wa kwanza wa kike Emiliana na wa pili Septemba 23, 1988 Linus na kwamba maisha yao awali yalikuwa ya upendo.

Anadai kuwa kabla ya hapo, Dk Slaa alikuwa padri lakini kwa ridhaa yake aliacha kazi hiyo ili aishi na familia yake na kutimiza majukumu yake katika ndoa hiyo.

Anaendelea kudai kuwa kuanzia hapo yeye na mdaiwa waliishi nyumba moja baada ya Dk Slaa kuacha utumishi wa Mungu kama mke na mume na walitambuliwa kuwa wanandoa, kwa sababu taratibu zote za ndoa zilifuatwa na familia zote mbili ambazo zinatambua hilo.

Alitaja kuwa katika mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na nyaraka kama hati za kusafiria zinawatambulisha kama mke na mume halali.

“Mdai na mdaiwa wa kwanza (Dk Slaa) waliishi maisha ya ndoa kwa amani, furaha na kuunganisha nguvu zao kwa ajili ya manufaa ya familia yao hapo baadaye na walichuma mali zikiwamo nyumba ya Sinza, Dar es Salaam katika kiwanja namba 609 Block E.

“Pia nyumba iliyoko Karatu katika kijiji cha Gongali ambayo ilijengwa mwaka 2005 pamoja na samani mbalimbali za nyumbani,” sehemu ya hati hiyo ilisema. Aidha, anadai mambo yalibadilika mwaka 2009 baada ya Dk Slaa kuanza uhusiano na Josephine, na hivyo kutotimiza majukuu yake kama mume na kulala nje ya nyumba akitumia mali za familia kutimiza maisha ya anasa na Josephine.

“Tangu mwaka 2009 mdai amekuwa akitunza familia peke yake bila msaada akijitunza mwenyewe na watoto hao wawili kwa kila kitu, ikiwa ni pamoja na ada za elimu ya juu za mtoto wa kwanza Emiliana akiwa Chuo Kikuu cha Ardhi mwaka wa mwisho akichukua Shahada ya Usimamizi wa Ardhi na Linus ambaye hivi karibuni amemaliza mafunzo ya Stashahada ya Tehama katika Chuo cha Tehama cha Learn cha Dar es Salaam,” ilidai hati hiyo.

Anaiomba Mahakama itamke kuwa ndoa inayotakiwa kufungwa Karatu au kokote na tarehe yoyote ni batili hivyo imwamuru Dk Slaa alipe Sh milioni 50 kama gharama ya kutunza familia kwa kipindi chote hicho na Josephine alipe Sh milioni 500 kwa uzinzi uliosababisha mumewe atelekeze familia.

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate