
Akichangia mada ya “Uongo” ndani ya kipindi cha Action & Cut cha Channel Ten hivi karibuni, Kingwendu alisema hata muigizaji Lulu (Elizabeth Michael) kesi yake imezingirwa na utata wa umri kutokana na kile kile alichokiita uongo wa wasanii wa kibongo.
“Mtu kwenye kadi ya benki jina lingine umri mwingine, kadi ya kupigia kura jina lingine umri mwingine, leseni ya kuendeshea gari jina lingine umri mwingine, what is this?” alishangaa Kingwendu.
Kingwendu alisema hata kwenye kumiliki vitu wasanii wengi hawasemi ukweli na ndo maana hata kwa marehemu Kanumba kulikuwa na utata mwingi juu ya mali alizoziacha.Msanii huyo aliwataka wasanii kuwa wakweli kuanzia kwenye majina, umri na mali wanazomiliki ili kuondoa utata.
(CHANZO CHA HABARI www.saluti5.com).
No comments:
Post a Comment