Pages

Thursday, November 8, 2012

MAN UTD YATINGA MTOANO, MESSI AWEKA REKODI MPYA.

AKITOKEA benchi, mshambuliaji Robin Van Persie, aliirudisha mchezoni Manchester United kwa kuisawazishia bao dakika ya 80 na kuchochea ushindi wa bao 3-1 dhidi ya Sporting Braga katika moja ya mechi za klabu bingwa ya Ulaya zilizochezwa usiku wa jana kuamkia leo.

Braga walitangulia kupata goli kutokana na penalti ya kubebwa dakika ya 49 kupitia kwa mshambuliaji wake Alan huku mabao mengine ya Manchester United yakifungwa na Rooney (penalti dak ya 84) na Chicharito dakika ya 90.
Kwa ushindi huo United imefanikiwa kuingia hatua ya mtoano kwa kujikusanyia pointi 23 ambazo haziwezi kufikiwa na timu yoyote ile.
Matokeo ya kushangaza zaidi ni yale yaliyoshudia Barcelona ya Hispania iliyotawala mchezo kwa asilia 79 ikilala kwa bao 2-1 dhidi ya Celtic ya Scotland.
Barcelona iliyokuwa nyuma kwa bao 2-0 hadi dakika ya 90 kwa mabao ya Victor Wanyama na kinda Tony Watt, ilijikuta ikitibua rekodi yake ya miaka mitatu ya kutofungwa katika hatua za makundi.
Messi aliyefunga bao la kufutia machozi alifanikiwa kuweka rekodi mpya ya kufunga magoli mengi zaidi ya ugenini (magoli 25) katika ligi ya mabingwa na kumpiku Ruud Van Nestroy aliyekuwa na mabao 24.
Matokea mengine katika mechi za jana ni Chelsea 3 -2 Shaktar, Benfica 2 – 0 Spartak Moscow, Juventus 4-0 FC Nordsjaelland, Bayern Munich 6 – 1 Lille, Valencia 4 – 2 Bate Barlov, CFR Cluj 1 – 0 Galatasaray 3.

No comments:

Post a Comment