Pages

Thursday, March 21, 2013

SIKU YA JANA LWAKATARE ARUDISHWA RUMANDE, MBWA WAWATULIZA WAFUASI WA CHADEMA

Wakili anayemtetea Wilfred Lwakatare, Peter Kibatara (kulia), akimueleza jambo Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe.
Mbowe akiwaeleza wanahabari njama za serikali kutaka kukidhoofisha chama chake.
Wakili Kibatara akiwafafanulia jambo wanahabari.
Mbowe akimtuliza mke wa Lwakatare baada ya mumewe kushindwa kutoka kwa dhamana.
Kikosi cha mbwa kikiwa tayari baada ya wafuasi wa Chadema kuanza kupiga mbiu za "Pipoooz.."
Mbwa wa polisi akiwaangalia wafuasi wa Chadema (hawapo pichani) kwa 'uchu'.
Askari magereza nao walikaa mkao wa kazi.
Kila mmoja akitawanyika kivyake baada ya mkwara wa polisi.
Jana asubuhi mbwa wa polisi waliwatuliza wafuasi wa Chadema waliofika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar kusikiliza kesi ya ugaidi inayomkabili Mkuu wa Kitengo cha Ulinzi na Usalama wa Chama hicho, Wilfred Muganyizi Lwakatare. Polisi wa kikosi cha mbwa na vikosi vingine walikaa tayari kuwadhibiti wafuasi hao walioanza kupiga mbiu ya chama hicho ya "Pipooooz..." baada ya kiongozi wao kushindwa kutolewa kwa dhamana. Lwakatare amerudishwa tena rumande baada ya kufutiwa mashitaka yake yote yanayomkabili na baadaye kukamatwa na kurudishwa rumande. Kesi yake itatajwa tena Aprili 3, mwaka huu.
(PICHA ZOTE NA RICHARD BUKOS / GPL)

No comments:

Post a Comment