Pages

Wednesday, April 24, 2013

MWANAFUNZI WA CHUO CHA UHASIBU ARUSHA ACHOMWA KISU NA KUPOTEZA MAISHA SDA NJIRO.

Mwanafunzi Henry Kova wa chuo cha Uhasibu(IAA) Arusha mjini mida ya saa nne usiku amechomwa kisu na watu wasiojulikana kwa tetesi za wana 2jiachie tumeongea na marafiki wa karibu wa marehemu wameweza kututonya kuwa marehemu Henry Kova alikuwa na begi alipokuwa akitoka chuo mida ya saa nne usiku wa jana.
                                                  Picha ya marehemu Henry Kova
Mwanafunzi huyu alikutwa na majanga hayo maeneo ya SDA njiro kilometa chache kutoka chuoni hapo.Eneo la SDA ni  masikani ya Vibaka kutoka Ungalimited na sehemu nyingine za Arusha na sio mara ya kwanza kutokea majanga eneo la Sda Arusha.
Kwa mujibu wa Rais wa chuo cha Uhasibu Arusha amesema kuwa marehemu Henry Kova alivamiwa na watu wasiojulikana  maeneo ya SDA na kumkwapua begi lake,kachomwa kisu na kupelekea kupoteza maisha.
 
Chanzo chetu kimeweza kuongea na baadhi ya wanafunzi wameonyesha kuingiwa ha hofu kubwa na wengine wakisema kuwa wanaunda kikosi cha kupanbana na watu wa aina hii maeneo ya SDA.

Habari zaidi kuwajia baadae......
CHANZO CHA HABARI NI 2JIACHIE

No comments:

Post a Comment