Pages
▼
Thursday, July 31, 2014
LOGARUSIC ATANGAZA WANACHOTAKIWA KUFANYA WACHEZAJI WAPATE NAMBA FIRTS XI SIMBA
Kocha wa Simba, Zdravko
Logarusic amesema hadi sasa kikosi chake hakika mchezaji mwenye uhakika na
namba.
Loga raia wa Croatia amesema wachezaji wote wanapaswa kujua sasa ndiyo wakati wa kusaka namna.
“Siwezi kuwa na mchezaji
mwenye uhakika na namba katika kikosi, isipokuwa nampa nafasi kila mmoja
kutafuta nafasi.
“Kama mchezaji anataka namba,
basi apambane mazoezini, aonyeshe juhudi, aonyeshe atakuwa msaada kwa timu,”
alisema Logarusic.
Kocha huyo wa zamani wa
Gor Mahia amesisitiza suala la nidhamu na wachezaji kujituma kuwa dira ya
muongozo wa kazi zake.CHANZO: SALEHJEMBE.COM
TAMASHA LA MATUMAINI 2014, MASTAA WAELEZA WATAKAVYOKAMUA TAIFA

ITAKUWA balaa! Siku chache kuelekea kwenye Tamasha la Matumaini, Agosti 8, mwaka huu, mastaa kibao watakaolipamba jukwaa litakalofungwa ndani ya Uwanja wa Taifa jijini Dar, wameeleza jinsi gani
Yemi Alade
Diva wa muziki kutoka pande za Nigeria ambaye huwa habahatishi, amesema: “Nitawapagawisha mashabiki kwa kupiga nyimbo zangu zote kali ikiwemo iliyojizolea umaarufu kila kona ya Afrika, Johhny. Mashabiki wategemee kumuona Yemi akimaliza. Kati ya nyimbo ambazo nitazipiga ni Tangerine, Johnny, Bamboo, Birthday, Ghen Ghen Love na nyingine kibao.”
Ali Kiba
“Kwa mara ya kwanza, nitapanda jukwaa la Uwanja wa Taifa kuweka historia mpya. Mashabiki wengi ‘wamenimiss’, Agosti 8 itakuwa maalum kwa ajili yao. Wategemee ngoma kali kibao kutoka kwa mfalme wa Bongo Fleva niliyerudi kupangusa kiti changu na kukikalia,
“Nitagonga kali kama Dushelele, Single Boy, Run Dunia na mpya zinazobamba kwa sasa ambazo ni Mwana na Kimasomaso.”
Shilole
“Mashabiki wategemee kuona shoo ya nguvu,
hakuna anayebisha kwamba najua kuimba na kukitumia vyema kiuno changu.
Nitazipiga Chuna Buzi, Paka la Baa, Nakomaa na Jiji, Lawama na hii mpya
ya Namchukuwa.”watakavyolishambulia jukwaa.
R.O.M.A“Huwa sibahatishi katika shoo zangu, nitawainua mashabiki kwa kunyoosha kidole cha mwisho juu kwa kupiga ngoma kali kibao kama Tanzania, Mechi za Ugenini, Pastor, Mr. President pamoja na hii mpya ya Karibu Kwenye Karamu (KKK).
Navy Kenzo
“Tutawapagawisha mashabiki kwa staili ya Bokodo iliyotokea kujizolea umaarufu mkubwa. Ngoma kama Cheza Kizembe, Usinibwage, Chelewa (Bokodo) na hii mpya ya Aiyola ndizo zitakazosisimua zaidi siku hiyo.”
Juma Nature
“Huwa ushindi kwetu ni lazima, tutakamua Tatu Bila, Fitina, Nyama pamoja na ngoma mpya niliyomshirikisha Lady Jay Dee, Kama Jana.”
Scorpion Girls
“Sisi huwa hatubahatishi, unapomuona sehemu Isabela na Jini Kabula ujue timu nzima ya Scorpion Girls imetimia. Tutacheza na kuwaimbia nyimbo zetu kama Tanzania, Watuache na nyingine kibao.”
Madee
“Pale taifa nitakwenda kudhihirisha urais wangu wa Manzese, nitazipiga zote kali ikiwemo Pombe Yangu, Tema Mate Tuwachape na hii mpya ya Ni Shidaa, noma saaana!”
Meninah
“Nitawapagawisha kwa ngoma zangu kali kama Dream Tonight, Kacopy Kapaste na mpya ya sasa ambayo ni Pipi ya Kijiti. Tukutane pale taifa, Agosti 8 mwaka huu.”
JK ATUNUKIWA TUZO NYINGINE YA KIMATAIFA, NI YA KUWA NYOTA WA DEMOKRASIA AFRIKA
Kwa mujibu wa barua aliyoandikiwa Rais Kikwete na kupokelewa Ikulu, Dar Es Salaam, Rais Kikwete amekuwa mshindi wa kwanza, na kwa mbali kabisa, katika mchuano na marais watatu wa Afrika ambao walifikia mwisho mwa mchuano wa kuwania tuzo hilo.
MAJAMBAZI 10 WANAOUNDA MTANDAO HATARI WA UHALIFU NCHINI WAMETIWA MBARONI, SILAHA MBALIMBALI ZAKAMATWA
Silaha hizo ni bunduki tisa zikiwemo SMG tatu, bastola mbili, short gun nne na risasi 15 zilikamatwa.
Kamishna wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova, aliyasema hayo ofisini kwake kwenye mkutano na waandishi wa habari.
Majambazi hao wamekamatwa katika msako mkali unaoendelea jijini Dar es Salaam katika harakati za kuhakikisha kwamba maisha na mali za wakazi wa Dar es Salaam vinalindwa kikamilifu.
Katika msako huo watuhumiwa walisachiwa katika miili, makazi, na maficho yao na wakakamatwa na jumla ya silaha 9 kama ifuatavyo:-
SMG NO. 13975 ikiwa na risasi 11 na magazine 2
SMG 1 haikuwa na magazine na namba hazisomeki.
BASTOLA 1 aina ya LUGER yenye namba 5533K
BASTOLA 1 aina ya BROWNING yenye namba TZACR83494 S/No.7670 Na risasi 6 ndani ya magazine.
HOYCE TEMU AHAMASISHA WATANZANIA KUMPIGIA KURA MISS TANZANIA USA 2014 KWENYE KINYANG'ANYIRO CHA MISS AFRICA USA
Pichani
ni Miss Tanzania USA 2014, Joy Kalemera katika pozi kabla ya mahojiano
na Mtangazaji wa kipindi cha "Mimi na Tanzania" Hoyce Temu nchin
Marekani.

Miss
Tanzania 1999 ambaye pia ni Mtangazaji wa kipindi cha "Mimi na
Tanzania" Hoyce Temu akipata ukodak na Miss Tanzania USA, Joy Kelemera
baada ya mahojiano maalum nchini Marekani.
Let us all wish her all the best! Ushindi wake ni wa Nchi! Piga Kura Sasa!
Pichani ni Hoyce Temu, Joy Kalemera na camera crew/IskaJojo studios (katikati) aliyefanikisha kukerokodi maojiano hayo.
SKYLIGHT BAND YAFUNIKA MBAYA EID MOSI NDANI YA ESCAPE ONE!
Sam
Mapenzi (katikati) akitoa burudani kwa mashabiki wa Skylight Band ndani
ya fukwe za Escape One katika show maalum kwa ajili ya kusheherekea
sikukuu ya Eid-El Fitr huku akipewa back Vocal na Sony Masamba pamoja na
Aneth Kushaba AK47.
Aneth
Kushaba AK47 akifanya yake jukwaani kuwapa raha mashabiki wa Skylight
Band katika kusheherekea sikukuu ya Eid El Fitr kwenye ukumbi wa Escape
One.
Mashabiki wa Skylight Band mdogo mdogo wakiachia kwenye dancing floor.
Sam
Mapenzi akitoa burudani adimu mashabiki wa Skylight Band katika sikukuu
ya Eid El Fitr kwenye kiota cha Escape One jijini Dar.
Skylight Band ni #balsaa# hebu angalia mashabiki wanaojua burudani ya muziki wa Live wanavyosebeneka.
Rappa
Mkongwe Joniko Flower akitunzwa wekundu wa msimbazi na mmoja wa
mashabiki wa Skylight Band aliyekunwa na uimbaji wa rapa huyo.
Binti mwenye sauti ya kumtoa Nyoka pangoni Mary Lucos akiwapa raha mashabiki wa Skylight Band (hawapo pichani).
Wednesday, July 30, 2014
GARI LA DUDE LAKAMATWA DAR KWA UJAMBAZI

GARI la muigizaji maarufu wa filamu Bongo, Kulwa Kikumba ‘Dude’ limekamatwa na Polisi jijini Dar es Salaam likihusishwa na tukio la ujambazi linalodaiwa kutokea Kijitonyama Mpakani usiku wa saa 5.15 Julai 21 mwaka huu.
Kwa mujibu wa chanzo chetu cha kuaminika, gari hilo aina ya Vitz lenye namba za usajili T 360 BAJ,
lilikutwa likiwa na vijana wawili ndani yake, waliotajwa kwa majina ya
Seif Jafari na Longina Ramadhani, waliotaka kupora Bajaj yenye namba za
usajili T 296 CSC iliyokuwa ikiendeshwa na Seleman Khalfani.
ABOUBAKAR SADIK APASULIWA
MSANII ANASWA CHINA

HUKU modo maarufu Bongo, Jacqueline Fitzpatrick Cliff ‘Jack Patrick’, akisota jela nchini China kwa skendo ya kukamatwa na madawa ya kulevya (unga), mrembo mwingine ambaye aliwahi kujaribu kuchomoka kisanii kwenye muziki wa Kizazi Kipya almaarufu kwa jina la Winnie Mandela, naye amenaswa na polisi nchini humo.

Tuesday, July 29, 2014
MTOTO ALIYETESWA SIKU 730 ATOROSHWA
YATIMA AOTA NYAMA YA AJABU ANA UMRI WA MIAKA 16 KILA ANAYEMLEA HUFARIKI DUNIA

Kwa kweli duniani kuna mateso, lakini ya mtoto huyu yatima ni makali na maisha yake yapo hatarini kama hatawahi kupata matibabu. Fuatilia mkasa wake hapa chini ambao naamini utakuhuzunisha.
Kijana Twaha Sultan (16) ambaye ni yatima mkazi wa Kipawa Karakata, Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam akisimulia mkasa wake alikuwa na haya ya kusema:
“Ndugu zangu, kufuatia maradhi ya ajabu yanayonisumbua sina raha ya maisha, niheri ningewafuata wazazi wangu waliotangulia mbele ya haki nikapumzike.“Nimekuwa mtu wa maumivu wakati wote, kulala na kula kwangu ni shida tupu mbaya zaidi ndugu ninaoishi nao hawana uwezo.
JK KATIKA SWALA YA IDDI DAR ES SALAAAM
Baadhi ya waumini wa dini ya kiislamu wakiswali sala ya Iddi El Fitr katika masjid Maamur Upanga jijini Dar es Salaam leo asubuhi.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na baadhi ya waumini wa dini ya kiislamu muda mfupi baada ya kuswali sala ya Iddi El Fitr katika mshikiti wa Maamur Upanga jijini Dar es Salaam leo asubuhi.
RAIS WA MAREKANI BARACK OBAMA AZUNGUMZA NA VIONGOZI VIJANA TOKA BARANI AFRIKA.
Ukumbi wa Regency Ballroom katika Hotel ya Omni Shoreham Washington DC ukiwa umepambwa kwa Bendera toka mataifa mbalimbali ikiwemo Tanzania.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani John Kerry akitoa hotuba yake kwa Viongozi vijana toka barani Afrika waliokuwa wakishiriki mafunzo katika vyuo vikuu vya Arkansas na Florida nchini Marekani.
Rais wa Marekani ,Barack Obama akizungumza na Viongozi vijana toka nchi mbalimbali za Afrika waliokuwa wakipata mafunzo katika vyuo vikuu vya Arkansas na Florida.
SWALA YA IDDI MKOANI ARUSHA LEO


Waumini wa dini ya kiislamu wakihitimisha mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani wakiwa kwenye ibada ya swala ya Iddy el Fitry kwenye uwanja wa sheikh Amri Kaluta Abeid jijini Arusha. Picha na Mahmoud Ahmad wa Globu ya Jamii, Arusha.
Monday, July 28, 2014
DEJAN LOVEN ATUA LIVERPOOL KWA DAU LA REKODI TANGU TIMU IANZISHWE
BEKI wa kimataifa wa Croatia, Dejan Lovren amekamilisha uhamisho wake kutua Liverpool kwa dau la Pauni 20 kutoka Southampton.
Sasa
mchezaji huyo anaweka rekodi ya kuwa beki ghali zaidi kuwahi kusajiliwa
na Wekundu hao wa Anfield akipiku dau la Pauni Milioni 18.6, ambalo
Liverpool ililipa kumsajili beki wa Paris St Germain, Mamadou Sakho
Septemba mwaka jana.
Lovren,
ambaye amekuwa mlengwa chaguo la kwanza la beki wa kati katika mawindo
ya kocha Brendan Rodgers dirisha hili la usajili, amesaini mkataba wa
miaka minne baada ya kufuzu vipimo vya afya Merseyside.