EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Friday, September 4, 2015

Masaburi aibuka sakata la vijana kuandamana

  Polisi wafanya upelelezi kubaini ni wa chama gani.
Mgombea Ubunge Jimbo la Ubungo kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Dk. Didas Masaburi.
Mgombea Ubunge Jimbo la Ubungo kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Dk. Didas Masaburi (pichani), amekanusha taarifa za kufadhili vijana wanaodaiwa kuandamana wakipinga aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kuondoka ndani ya chama hicho. 
 
Dk. Masaburi alikanusha taarifa hizo jana wakati akizungumza na  waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuhusiana na uvumi uliozagaa kwenye mitandao ya jamii kuwa vijana 10 wanaoshikiliwa na Jeshi la Polisi kwa sababu ya kuandamana bila ya kibali wakimtaka Dk. Slaa asiondoke kwenye chama hicho walitumwa na yeye.
 
“Tuhuma hizo si za kweli, hata kama ninaunga mkono hoja zilizotolewa na Dk. Slaa kuhusiana na tuhuma za ufisadi dhidi ya viongozi waliohamia Chadema kutoka CCM, lakini siwezi kufadhili maandamano ya wanachama wa Chadema ya kushinikiza  kubakia kwa Dk. Slaa ndani ya chama hicho,” alisema.
 
Alisema vijana aliowapokea katika ofisi ya CCM Jimbo la Ubungo zilizoko Manzese juzi baada ya kurudisha kadi za vyama vyao kikiwamo cha Chadema walifanya hivyo kwa mapenzi yao wakisema wamechoshwa na hadaa katika vyama walivyotoka. Aidha, Dk. Masaburi aliwataka viongozi wa Chadema kujibu hoja zilizotolewa na Dk. Slaa badala ya kutafuta mchawi baada ya kuona amewaumbua na wanachama wao wanakihama chama hicho.
 
Wakati huohuo, Jeshi la Polisi mkoa wa Kinondoni, jijini Dar es Salaam limesema linaendelea na upelelezi ili kubaini vijana walioandamana juzi eneo la Morocco, jijini humo iwapo ni wanachama wa Chadema au  la.
 Juzi vijana takribani 100 wanaodaiwa kuwa wanachama wa Chadema waliandamana katika eneo hilo wakishinikiza kurudi katika chama hicho kwa aliyekuwa  katibu mkuu wake, Dk. Willibrod Slaa, ambaye alitangaza kujitoa na kujitenga na siasa, huku  akimtuhumu mgombea urais wa chama hicho, Edward Lowassa, masuala mbalimbali ua ufisadi.
 
Kamanda wa Polisi wa kanda ya Kinondoni, Camilius Wambura kupita msaidizi wake, jana aliliambia Nipashe kuwa bado wanawashikilia vijana 10 kati ya 100 ambao walitawanywa kwa mabomu ya machozi baada ya kukaidi amri ya jeshi hilo ya kutakiwa kutawanyika, huku wakiendelea na upelelezi kubaini wanatoka chama gani.
CHANZO: NIPASHE

1 comment:

  1. MKUU WA MKOA WA DARESSALAAM UMETUMMWA NA NANI KUFYATUKA HIVO? UNATUTIA HASIRA SANA SANA SIKU YA .UNASEMA WAMEANDALIWA VIJANA KUFANYA FUJO SIKU YA KUPIGA KURA.TUNAJUA UNAWALENGA UKAWA YA EDWARD LOWASSA.UMEANZA KUWATIA HOFU WAPIGA KURA HASA AKINA MAMA.HAYO NI MATAMSHI YA UOVU,NA NDIYO MAKUANA KAMANDA WA POLISI KANDA MAALUM YA DARESSALAAM KAMANDA KOVA AMEKUJIBU KUWA POLISI HAIKUA NA HABARI HIZO KWA HIYO NI UZUSHI -UMEZUA-WAKATI UKAWA WANAOMBA KWA MWENYEZI MUNGU AMANI ITAMALAKI TANZANIA ILI SIKU ILE YA UCHAGUZI WANANCHI WAMPE LOWASSA DOLA KWA KUPITIA SANDUKU LA KURA KWANI WANANCHI WAPIGA KURA ZAIDI YA ASILIMIA 80 WAMEKWISHA AMUA MECK SADICK ANAANDAA UVCCM KUFANYA FUJO VISINGIZIO VYA KISHETANI.TUMEKWISHA AMUA KUMPA MHE.LOWASSA NCHI KWA AMANI NA UTULIVU KUPITIA SANDUKU LA KURA

    ReplyDelete

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate