Pages
▼
Wednesday, December 16, 2015
Kajala ajiachia na dada’ke diamond!

Mwigizaji Kajala Masanja akiwa na Queen Darleen wakiponda raha.
Na Musa MatejaHUKU kukiwa na madai kwamba mwigizaji Kajala Masanja ana uhusiano wa ‘kikubwa’ na Mbongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, mwigizaji huyo amezidi kuyachochea moto madai hayo kwa kutokana na kujiachia mara kwa mara na dada wa Diamond, Queen Darleen, Risasi Mchanganyiko linakujuza.
Kwa mujibu wa chanzo makini, Kajala na Queen Darleen wamekuwa ‘beneti’ kila kona ambapo pia kuna fununu kuwa hata familia ya Diamond imebariki uhusiano wake na Mbongo Fleva huyo na wanampa ushirikiano wa kutosha Kajala.
“Fuatilieni tu, Kajala ameshakubalika kwa kina Diamond, ndiyo maana leo utaona Kajala na dada yake Diamond, Queen Darleen wanapiga misele pamoja, hata katika viwanja vingi vya starehe wanakwenda wote,” kilisema chanzo hicho.

…..Wakifurahia jambo.
Mwishoni mwa wiki hii, paparazi wetu aliwanasa laivu Kajala na Queen
Darleen katika fukwe za White Sands, Mbezi Beach jijini Dar es Salaam
walipokuwa wameenda kupunga upepo na kuwapeleka watoto wao kuogelea.Kuonekana kwa wawili hao kuliibua gumzo la aina yake ambapo wafuatiliaji wa ‘ubuyu’ walionekana kunong’onezana kuwa yale waliyokuwa wakiyasikia na kuyasoma kwenye mitandao kuwa Kajala ana uhusiano na Diamond, yana ukweli.

Ili kukamilisha ubuyu huo, mwanahabari wetu alimuibukia Kajala aliyekuwa ameambatana na mwanaye Paula pamoja na baunsa wake, ili aweze kuzungumzia ukaribu wake huo na Queen ambao umeleta tafsiri kuwa ni mtu na wifi yake. Kajala akafunguka:

Kwa upande wake, Queen Darleen alisema mwenye macho haambiwi tazama!
CHANZO: GPL
Friday, December 11, 2015
Rayuu afungukia kujiuza nje
Msanii wa filamu Bongo, Alice Bagenzi ‘Rayuu’.
MAYASA MARIWATAMSANII wa filamu Bongo, Alice Bagenzi ‘Rayuu’ amefungukia ishu ya mastaa wengi kupenda kwenda kujiuza nchi za nje ikiwemo Sauzi akisema kuwa, wanaofanya hivyo hawajitambui na kinachowasumbua ni tamaa ya pesa.
Akipiga stori na paparazi wetu hivi karibuni, Rayuu alisema alishasumbuliwa na wadada wengi wakimpa madili ya kwenda kujiuza China, Sauzi na kwingineko lakini akawatolea nje kutokana na msimamo alionao
“Unajua hakuna kinachowapeleka huko zaidi ya tamaa kwa kuwa kule wanalipwa kwa dola wakirudi huku wakizibadilisha wanapata pesa nyingi, halafu huku unakuta mtu ameshatembea na wanaume wengi ndiyo maana anakimbilia nje,” alisema Rayuu.
Bodi ya Mikopo watoa awamu ya pili wanafunzi waliopata mkopo 2015/16
AWAMU YA PILI YA WANAFUNZI WALIOPANGIWA MIKOPO KWA 2015/2016
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) inapenda
kuwafahamisha waombaji wa mikopo kwa mwaka wa masomo 2015/2016 kuwa
imetoa Awamu ya Pili ya waombaji 28,554 waliofanikiwa kupata mikopo na
kufanya idadi ya waombaji wenye sifa wa mwaka wa kwanza waliofanikiwa
kupata mikopo hadi sasa kufikia 40,836.Katika awamu ya kwanza, Bodi ilitoa orodha yenye jumla ya waombaji 12,282 waliofanikiwa kupata mikopo.
Majina ya waombaji waliofanikiwa kupata mikopo kutoka katika awamu zote mbili yanapatikana kupitia mtandao wa Bodi wa olas.heslb.go.tz na tovuti ya Bodi (Bofya Hapa www.heslb.go.tz ) Aidha, orodha hizo pia zimetumwa vyuoni kwa ajili ya taratibu za usajili.
Lengo la Bodi ni kuhakikisha kuwa wanafunzi wa mwaka wa kwanza wenye sifa ya kupata mikopo katika mwaka wa masomo 2015/2016 wanapata mikopo na hivyo kupata elimu ya juu.
Aidha, Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu inapenda kuwasihi waombaji wa mikopo kuwa watulivu na kupuuza taarifa zinazosambaa katika baadhi ya mitandao ya kijamii kuwa Bodi haitatoa mikopo kwa waombaji kwa mwaka wa masomo 2015/2016.
Imetolewa na:
MKURUGENZI MTENDAJI
BODI YA MIKOPO YA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU
09 November 2015
Paul Makonda azindua Bahati Nasibu ya Shinda Nyumba kutoka Global

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul
Makonda (katikati) akizindua Bahati Nasibu ya Shinda Nyumba
inayoendeshwa na Kampuni ya Global Publishers Ltd. Kulia ni Meneja Mkuu
wa Global Publishers Ltd, Abdallah Mrisho na kushoto ni Mkurugenzi
Mtendaji wa Global Publishers Ltd, Eric James Shigongo.
Paul Makonda akigawa vipeperushi vyenye nyumba na zawadi nyingine zinazoshindaniwa kwa wanahabari.

Meneja Mkuu wa Global Publishers Ltd,
Abdallah Mrisho akiwakaribisha wanahabari na Mkuu wa Wilaya ya
Kinondoni, Paul Makonda katika uzinduzi wa Bahati Nasibu ya Shinda
Nyumba uliofanyika katika ofisi za Global zilizopo Mwenge, Bamaga jijini
Dar.