Pages

Wednesday, March 16, 2016

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL), David Mattaka Ashitakiwa Tena Kwa Uhujumu Uchumi


Mkurugenzi Mtendaji wa zamani wa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), David Mattaka na wenzake wawili wamepandishwa kizimbani wakikabiliwa na mashtaka sita yakiwamo ya matumizi mabaya ya madaraka, kughushi na kuisababishia hasara Serikali kupitia ukodishaji wa ndege.

Wakili Mkuu wa Serikali, Timon Vitalis akishirikiana na mawakili wa Takukuru, Joseph Kiula na Stanley Luoga waliwataja washtakiwa wengine wanaokabiliwa na kesi hiyo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Respicius Mwijage kuwa ni Ofisa Mtendaji Mkuu Mstaafu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Manunuzi ya Umma (PPRA), Ramadhan Mlinga na Mwanasheria wa mamlaka hiyo, Bertha Soka.

Wakili Vitalis alidai kuwa Oktoba 9, 2007 katika ofisi za ATCL zilizopo wilayani Ilala, Mattaka alitumia vibaya madaraka kwa kutia saini mkataba wa ukodishaji wa ndege A320-214 iliyotengenezwa kwa namba 630 baina ya Wallis Trading Inc na ATCL.

Husna, Mobeto ndani ya bifu zito

DSC_0490Husna Maulid.
Na Mwandishi wetu RISASI mchanganyiko
DAR ES SALAAM: Bifu la chinichini linaendelea kuwatafuna warembo wawili ambao wote waliwahi kunyakua taji la urembo wa Miss Kinondoni kwa nyakati tofauti, Husna Maulid (pichani)na Hamisa Mobetto baada ya kudaiwa kumgombea bwana, ambaye ni raia wa DRC, aitwaye Mwami Rajabu.
Chanzo chetu makini kilisema kuwa Husna ndio wa kwanza kuanza kumtuhumu Hamisa kuingilia mapenzi yake na mtu wake huyo wa muda mrefu, kiasi cha kuanza kurushiana vijembe vikali mpaka kwenye mtandao wa kijamii wa Instagram.
Mpashaji wetu alizidi kuweka wazi kuwa wakati Hamisa akirusha vijembe, Husna mara nyingi amekuwa sio mzungumzaji zaidi  ya kuangalia mchezo unavyokwenda huku akiwaambia baadhi ya marafiki zake hataki kumpa kiki mrembo huyo.
IMG-20160311-WA0003Hamisa Mobeto akiwa na Mkongo.
“Mara nyingi Mobeto amekuwa sio mtu wa kuzungumza kabisa  na kila wakati anawaambia marafiki zake kuwa hataki kabisa kumpa kiki Husna kwa kumjibu chochote kile”
Gazeti hili liliwaendea hewani wasichana hao wawili, lakini Husna aliposomewa mashtaka yake alisema yeye Hamisa na mambo yake hivyo hawezi kumfuatilia.
“Hamisa ana mambo yake bwana  achana naye, ana mambo ya kisichana.”
Kwa upande wake, Hamisa alisema yeye anaona kama Husna ndio anamchokonoa, kwani yeye anajiheshimu na hayuko tayari kumpa mtu kiki kwa kugombana naye kwa vyovyote vile.
“Mimi sasa hivi ni mama na vitu vingi keshafanya huyo Husna, ila mimi nanyamaza sipendi kumpa mtu faida maana mtu anapokuona una matatizo ndio hapohapo anapotafuta sababu  ambazo hazina maana,”alisema Hamisa.