Mkurugenzi
wa Vipindi na Uzalishaji wa Clouds Media Group, Ruge Mtahaba akifungua
Semina ya Kamata Fursa Jitathimini, Jiamini kisha Jiongeze mapema leo
kwenye Ukumbi wa Bwaro la Magereza mjini Musoma.
Mkuu wa Mkoa wa Busega, Paul Mzindakaya akiwaonyesha fursa mbalimbali wakazi wa Musoma.
Msanii wa Muziki wa Dansi nchini, Christian Bella akitumbuiza kwenye semina ya Kamata Fursa.
Msanii Hip Hop Bongo, Nikki wa Pili akizungumza neno kwenye semina ya Kamata Fursa.
Baadhi ya wakazi wa Musoma wakifuatilia kwa makini semina ya Kamata Fursa ndani ya Ukumbi wa Bwalo la Magereza.
Mkuu wa Wilaya ya Busega, Paul Mzindakaya akiteta jambo na Ruge wakati semina ya Kamata Fursa ikiendelea.
Nay wa Mitego akiingia kwenye semina ya Kamata Fursa ndani ya Bwalo la Magereza mjini Musoma.
Mtangazaji wa kipindi cha Jahazi cha Clouds FM, Mussa Hussein akizungumza jambo kwenye semina hiyo.
Msanii
Lameck Ditto akiwapa mbinu mbalimbali wakazi wa Musoma ili wapate
kujikwamua kiuchumi kama alivyoweza yeye kupigania maisha yake.
Baadhi ya umati uliyojitokeza ukumbini hapo ukifuatilia kwa makini semina hiyo.
MPANGO wa Serengeti Fiesta Kamata Fursa leo
umefanyika kwa mara ya kwanza kwa wakazi wa mji wa Musoma ambapo baadhi
ya watu mashuhuri walipata nafasi ya kuongea na wakazi hao na kuwapatia
mbinu mbalimbali watakazoweza kufanya kwa ajili ya kujikwamua katika
shughuli zao za kiuchumi.
Akizindua Semina ya Kamata Fursa Twenzetu, Mkurugenzi wa Vipindi na
Uzalishaji wa Clouds Media Group, Ruge Mtahaba alisema kuwa, leo ilikuwa
ni siku mwafaka kwa kuwaonyesha fursa mbalimbali zilizopo mjini Musoma.
Kwenye Semina hiyo pia Mkuu wa Wilaya ya Busega, Paul Mzindakaya
alipata fursa ya kuzungumza na wakazi wa Musoma na kuwapatia mbinu
mbalimbali zitakazowawezesha kujikwamua kimaisha kupitia njia ya
biashara ya kilimo cha kila mwaka.
Pia msanii wa Bongo Fleva, Lameck Ditto naye alipata muda mwafaka wa
kuzungumza kwa kifupi na wakazi wa mkoa huo na kuwataka waongeze bidii
kwenye shughuli zao za kila siku kwa kuwa anaamini mafanikio ya mtu
yanatokana na juhudi binafsi, ikiwa ni pamoja na kutumia rasilimali
mbalimbali zilizopo sehemu husika.
(HABARI/PICHA: MUSA MATEJA/ GPL, MUSOMA)
No comments:
Post a Comment