Dk
Ulimboka.Mwenyekiti wa Jumuiya ya madaktari nchini, Dk Stephen Ulimboka
amelazwa katika hospital ya Taifa ya Muhimbili baada ya kuokotwa katika
pori la Pande nje kidogo ya jiji akiwa taaban.Inasemekana Dk Ulimboka
alitekwa jana na watu wasiojulikana.
Serikali inawajibika kutueleza: Dkt. Ulimboka kutekwa, kupigwa na kuumizwa - Zitto Kabwe
Ujumbe amenitumia Daktari yupo pale MOI
‘Kaka
Zitto,hali ya Dr.Ulimboka yuko unconscious,multiple ribs fracture na
kwenye mikono pia amevunjika pamoja na taya,yuko icu wanamstabilise
kwanza kwasababu hapumui vizuri,the situation here is really bad, I
agree with you this is outright outrageous’
Nimechukizwa
sana na habari za kutekwa, kupigwa na kuumizwa vibaya kwa Dr Ulimboka,
Kiongozi wa Madaktari Nchini. Mambo kama haya tumezoea kuyasikia kwenye
nchi za kidikteta na kuongozwa kiimla ambapo watawala badala ya kutumia
njia ya kidemokrasia na kisheria kushughulikia wanaoamini ni maadui zao
katika utawala, hutumia wahuni katika Taasisi za usalama kuteka raia,
kuwatesa, kuwafunga na hata kuwaua.
Sitaki
kuamini kwamba Tanzania imefikia huko. Nimezungumza na baadhi ya
madaktari walio karibu na Dokta Ulimboka na kujulishwa kwamba majeruhi
huyu wa vitendo vya hovyo kabisa kutokea hapa nchini alikamatwa jana
usiku mnamo saa sita na watu wasiojulikana na kupelekwa katika msitu wa
MagwePande na kujeruhiwa vibaya. Habari hizi bado hazijathibitishwa na
vyanzo huru lakini ndio zilizopo hadi hivi sasa.
Serikali
kama mlinzi wa usalama kwa raia inaWAJIBU kueleza tena kwa haraka ni
nini kimetokea kwa kijana huyu msomi na kiongozi wa wataalamu wenzake.
Serikali INAWAJIBIKA kueleza katika nyakati kama hizi ambapo kuna
mgogoro kati yake na madaktari imekuwa wapi kuhakikisha usalama wa
viongozi wa madaktari ili kuepusha watu wanaoitwa ‘agente provocateure‘ kuweza kuhatarisha hali ya amani ya nchi na hata kupelekea kuweka hali ya vitisho kwa madaktari wetu.
Serikali INAWAJIBIKA kueleza kama sasa imeamua kutumia njia za kihuni kumaliza matatizo na wananchi wake.
Nimemuomba
Waziri kivuli wa Afya wa CHADEMA kufuatilia suala hili kwa kwa karibu
sana ili kuhakikisha kwamba ukweli wote na ukweli mtupu unafahamika.
Kamwe hatuwezi kuacha Mtanzania yeyote aonewe, anyanyaswe au akandamizwe
eti kwa sababu ya kudai haki yake na za wenzake. ‘An injury to one,
injuries to all’
Naomba madaktari wamwangalie kwa karibu daktari mwenzao ili aweze kupata nafuu. Ulinzi uimarishwe ili kuhakikisha usalama wake.
Hali aliyokutwa nayo Dkt. Ulimboka
UPDATE ya maelezo ya mkasa uliomkuta Dkt. Ulimboka:
Dkt.
Helen Kijo-Bisimba wa LHRC akinukuliwa katika EA Redio amekariri
maelezo ya Dkt. Ulimboka ambayo pia yamesikika yakitamkwa na mwenyewe
(Dkt. Ulimboka Steven), kupitia kituo cha redio cha CloudsFM,
kwamba walikuja watu watatu waliovalia kiraia na kujitambulisha kuwa wao
ni askari. Watu hao walimchukua na kumuingiza katika gari lisilokuwa na
namba na kuanza kuelekea barabara ya Bagamoyo. Huko walimfunga kitambaa
usoni, kamba mikononi na miguuni kisha wakampiga huku
wakimwambia amekuwa akiwasumbua kwa muda mrefu na kama wangekuwa na
sindano ya sumu wangemmaliza kabisa.
---
UPDATE:
Dkt. Ulimboka amefikishwa katika hospitali ya Muhimbili kwa ajili ya kupatiwa huduma. Hali yake ni mbaya ila "stable".
------
Baadhi
ya watu wa shirika la Tanzania Legal Human Rights Center (LHRC)
walifanya juhudi za kumtafuta kiongozi wa Jumuiya ya Madaktari Tanzania,
Dkt. Ulimboka Steven aliyekamatawa (? tekwa) jana usiku.
Taarifa
iliyotoka kwa mmoja wa wanaharakati hao inasema, walifanikiwa kumpata
Dkt. Ulimboka kaitka eneo la Mwabepande, Dar es Salaam ) akiwa amefungwa
kamba miguuni na mikononi, hajitambui (unconscious) na asiyeweza
kuzungumza.
Taarifa hiyo inaongez akuwa, Dkt.
Ulimboka alikuwa amepigwa vibaya sana katika sehemu mbalimbali za mwili
wake na anahitaji matibabu ya haraka.
Juhudi zinafanywa kumpatia msaada unaohitajika Dkt. Ulimboka Steven.
No comments:
Post a Comment