Pages

Friday, June 29, 2012

Rose Ndauka akubalika Ghana

Kipaji cha kuigiza cha msanii nyota wa filamu za Tanzania, Rose Ndauka kimewakuna Waghana na kumtabiria kuwa msanii atakayekuja kuwa juu sana barani Afrika.
Kwa mujibu wa mtandao mmoja wa nchini humo, filamu za staa huyo zinanunuliwa kwa kasi ambapo amshabiki wengi walidhani ni msanii kutoka Nollywood kama si kubabaishwa na Kiswahili inayotumika kwenye filamu zake.

Miezi mitatu iliyopita, staa huyo alikwenda nchini Ghana kufanya kazi za filamu kwa kushirikiana na wasanii wa huko, kazi hizo zitaanza kuoneka na kwenye runinga za kimataifa hivi karibuni.
Kwa nchini Tanzania, Rose ambaye ni mchumba wa msanii wa Bongo Fleva, 
Maliki Bandawe, anazidi kufanya vizuri katika kazi zake za sanaa ambapo amefanikiwa kufungua kampuni yake ya kutengeneza filamu ya Ndauka Entertainment.
Kwa upande wa mchumba, Rose anatarajia kufunga ndoa mwaka huu ingawa tarahe haijapangwa. 

No comments:

Post a Comment