Pages

Monday, July 2, 2012

Hospitali ya Mt. Fransis, Morogoro yawafukuza kazi Madaktari 17

Uongozi wa Hospitali ya Rufaa ya Mtakatifu Francisco mjini Ifakara mkoani Morogoro, umewafukuza kazi madaktari 17, waliodaiwa kujihusisha na mgomo wa Madaktari unaoendelea nchini hivi sasa.

Madaktari hao, walifukuzwa chini ya ulinzi mkali wa askari polisi waliokuwa na silaha.

Tukio hilo, limetokea juzi jioni baada ya kukabidhiwa barua za kufukuzwa hospitalini na kutakiwa kukabidhi vifaa vya tiba na kuondoka kwenye nyumba za hospitali hiyo.

Mganga Mkuu wa Hospital hiyo, Dkt. Angelo Nyamtema alisema uamuzi huo ulifikiwa na uongozi wa Kanisa Katoliki Jimbo la Ifakara, baada ya kubaini makosa mbalimbali, yakiwamo ya kuchochea mgomo.

Barua mojawapo kati ya walizokabidhiwa madaktari hao ilisema hawatakiwi kuonekana katika eneo la hospitali kuanzia saa 12 jioni ya Juni 30.

Madaktari waliofukuzwa kazi ni Greyson Mpinga, Kasanzu Masanja, Haithan Mohamed, Masanja Dotto, Nicholaus Sayana, Kahibi Bernad, Emanuel Kimario, Rebeca Majige, Allen Kissanga, James Zakaria, Kurenje Mbura, Nyambura, Moremi, Donald Kennedy Elipokea Sarakikya, Magreth Kagashe, John Mrina na Sebastian Pima.

Awali, madaktari hao waligoma kupokea barua za kuondoka kwa madai kuwa mpaka jana hawakuwa wamekabidhiwa vyeti vyao.

Akizungumzia hali ya matibabu hospitalini hapo, Dk. Nyamtema alisema, hali ni shwari na wagonjwa wanahudumiwa kama kawaida

Merina Robert, MTANZANIA
Morogoro

No comments:

Post a Comment