Pages

Sunday, July 29, 2012

Kiburu, Ndafu, Shiro, Kitawa, Machalari, Ngararimo, Ng’ande, Kisusio, Mtori - CHAGGA DAY

Mkazi wa jiji la Dar es Salaam akimiminiwa Mbege katika "kipata", kata maalum la kunywea pombe hiyo ya asili ya Wachaga kutoka mkoani Kilimanjaro wakati wa tamasha maalum la CHAGGA DAY lililofanyika katika viwanja vya Lidaz jijini Dar es Salaam.

Wadau wakipata mbege wakati wa tamasha la CHAGGA DAY lilofanyika katika viwanja vya Leaders jijini Dar es salaam jana


Bendi ya Msondo Ngoma ikitoa burudani wakati wa tamasha la Chagga Day jana


Vimwana wa bendi ya Twanga wakionyesha umahiri wao wakiongozwa Luiza Mbutu wakati wa CHAGGA DAY.


Nyama choma ilikuwa ya kutosha

Masta wa tamasha la chagga day (katikati) Mkurugenzi wa Kampuni ya MyWayEntertainment, Paul Maganga pamoja na wadau wengine wakiwa kwenye picha ya pamoja.

Wadau wakifurahia utamu wa mbege.

Wadau mbalimbali wakipata mbege pamoja na vyakula vya kiasili kama mseto Kiburu, Ndafu, Shiro, kitawa, Machalari, Ngararimo, Ng’ande, Kisusio, Mtori na vingine vingi
picha zote via blogu ya Father Kidevu

No comments:

Post a Comment