Pages

Tuesday, July 3, 2012

Manji aibuka kidede TFF

 
KAMATI ya Uchaguzi ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) chini ya Mwenyekiti wake Deogratius Lyato, jana ilitupilia mbali pingamizi dhidi ya Yusuf Manji kuwania uenyekiti wa klabu ya Yanga.

Kwa mujibu wa taarifa ya Kamati hiyo iliyosainiwa na Lyato, wameamua hivyo kutokana na mrufani, Ishabakaki Luta kushindwa kutimiza matakwa ya kanuni za uchaguzi Ibara ya 11 (2).
Kwa mujibu wa ibara hiyo, mrufani anapaswa kuwasilisha vielelezo vya rufaa yake, anuani ya kudumu na saini yake.

Lyato amesema, mrufani ameshindwa kutimiza matakwa hayo ya kanuni pamoja na kushindwa kutokea kutetea hoja zake hiyo jana mbele ya Kamati ya Rufaa.
“Kwa kuwa mrufani hakutimiza matakwa ya kanuni ya uchaguzi ibara ya 11 (2) ambayo inamtaka mrufani kuweka vielelezo vya rufaa yake, anuani ya kudumu na saini yake.

“Kwa kuwa, mrufani hakutokea kutetea rufaa yake, kamati ya uchaguzi imetupilia mbali rufaa ya Ishabakaki Luta,” ilisema taarifa hiyo.
Kutupwa kwa rufaa hiyo dhidi ya Manji, kunampa tiketi ya kushiriki uchaguzi huo wa Julai 15, akichuana na wengine watatu kwenye nafasi hiyo.
Mbali ya Manji, wengine wanaowania nafasi hiyo, ni Sarar Ramadhani, John Jembele na Edger Chibula.
Wagombea wa nafasi ya Makamu, ni Ayoub Nyenzi, Stanley Kevela ‘Yono,’ na Clement Sanga.

Wanaowania ujumbe ni Lameck Nyambaya, Ramadhan Mzimba, Mohamed Mbaraka, Ramadhan Saidi, Edger Fongo, Beda Simba, Ahmed Gau, Mussa Katabalo na George Manyama.
Wengine ni Aaron Nyanda, Abdallah Bin Kleb, Omari Ndula, Shaaban Katwila, Jumanne Mwammenywa, Abdallah Mbaraka, Peter Haule, Justine Baruti na Abdallah Sharia.
Kwa mujibu wa ratiba ya uchaguzi huo mdogo wa kuziba nafasi sita zilizoachwa wazi kutokana na sababu mbalimbali, kampeni zinaanza leo.

Nafasi zinazowaniwa ni Mwenyekiti, Makamu na nafasi nne za ujumbe wa Kamati ya Utendaji; baada ya watatu kujiuzulu na mmoja kufariki.
Mwenyekiti Lloyd Nchunga alijiuzulu Mei 23 mwaka huu kwa shinikizo la Wazee na Vijana huku aliyekuwa Makamu wake, Davis Mosha alijiuzulu Machi, 2011.Habari na Dina Ismail

No comments:

Post a Comment