Pages

Tuesday, July 3, 2012

Mastaa wa Bongo waosha magari Arusha

 ROSE Ndauka na Jackie Wolper ni miongoni mwa mastaa wa kike wa filamu za Bongo waliothibitisha kushiriki tukio la kuosha magari litakalofanyika kwenye klabu ya Matongee mjini Arusha Julai 14.

Tukio hilo la hisani linalenga kuchangisha pesa kwa ajili ya kuwasaidia watoto walio katika mazingira magumu walio katika kituo cha kulelea watoto cha kilichopo nje kidogo ya jiji la Arusha.

Kituo hicho kinafahamika kama Good hope, kipo eneo la USA River nje kidogo ya jiji hilo kina watoto wapatao 50 wenye umri kuanzia mwaka na nusu hadi yani wanashida sana

Angel Justice ambaye ni msemaji wa tukio hilo alisema Ndauka amethibitisha kwamba atashiriki na bado wanaendelea kuzungumza na mastaa wengine.

Alisema mrembo Sylivia Shaali nae atashiriki kwa kuwaongoza warembo washiriki wa Kinyang anyiro cha Miss Arusha katika shughuli hiyo ya kijamii. Shughuli hiyo itaambatana na disco la aina yake litakaloporomoshwa na Jambo squad pamoja na wamamuziki wengine kibao kutoka ndani na nje ya Arusha alisema.Habari na
MAIMUNA KUBEGEYA

No comments:

Post a Comment