VIGOGO wawili wa Chama cha Maendeleo na Demokrasi (Chadema), leo
Jumatatu asubuhi wanatarajiwa kuburuzwa kizimbani katika mahakama ya
hakimu mkazi mjini hapakujibu tuhuma ya kumtolea lugha ya matusi Mbunge
wa Jimbo la Iramba Magharibi, Mwigullu Lameck Mwigullu.
Vigogo
hao ni pamoja naOfisa sera na utafiti wa ChademaMakao makuu,Waitara
Mwita Mwikwabe (37) na mshauri wa Chadema na Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha
Dar-es-salaam, DkKitila Mkumbo wotewakazi wa jijini Dar-es-salaam.
Washitakiwa hao kwa nyakati tofauti wiki mbili zilizopita,walipandishwa katika mahakama hiyo na kukana kutenda kosa hilo.
Kwa
mujiubu wa mwanasheria wa Serikali,Seif Ahmedalidai mbele ya hakimu wa
mahakama hiyo,Ruth Massamu kuwa Julai 14, mwaka huu saa 10.00 alasiri
huko katika kijiji cha Nguvumali kata ya Ndago wilayani
Iramba,washtakiwa bila halali alimtusi Mbunge Mwigullu kuwa ni
malaya,mzinzi na mpumbavu huku akijua wazi kuwa kitendo hicho ni kinyume
na sheria.
Seif alisema washitakiwa hao bila halali,alitenda
kosa hilo kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji cha
Nguvumali uliolenga viongozi wa Chama hicho kuzungumza na wananchi.
Pamoja
na vigogo hao, leo asubuhi vijana nane wakazi wa kijiji cha Nguvumali
ya Ndago,Jimbo la Iramba magharibi,wanatarajiwa kupandishwa katika
mahakama ya hakimu mkazi mjini hapa,wakituhumiwa kumw
uuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana (CCM) kata ya Ndago, Yohana Mpinga (30).
Washitakiwa
hao ni Manase Daudi (40),Williamu Elia (33),Frank Stanley (20),Charles
Leonard (36),Tito Nintwa, Fillipo Edward (30),Paulo Shakilingwa na
Emmanuel John Shilla (20).
Mwanasheria wa Serikali mwandamizi,
Neema Mwanda,alidai mbele ya hakimu Massamukuwa Julai 14 ,saa kumi
alasiri katika kijiji cha Nguvumali kata ya Ndago,washitakiwa wote kwa
pamoja,bila halali walimpiga kwa kutumia fimbo na mawe mwenyekiti
huyona kusababisha kifo chake.
Vile vile jumla ya washitakiwa 12
wanaotuhumiwa kufanya vurugu katika mkutano huo wa hadhara wa Chadema
katika kijiji cha Nguvumali kata ya Ndago na kusababisha kuvunjika kwa
amani na utulivu,nao wanatarajiwa kupandishwa kizimbani katika mahakama
ya hakimu mkazi mjini hapa.
No comments:
Post a Comment