Pages

Friday, August 31, 2012

MAMA HAWA NGULUME AFARIKI DUNIA.

Bi Hawa Ngulume enzi za uhai wake.
Bi Hawa Ngulume, aliyewahi kuwa Mkuu wa wilaya ya Kinondoni, Bagamoyo na Mbarali, amefariki dunia jijini Dar es Salaam jana asubuhi. Mama Ngulume ambae pia ni mama mwenye nyumba wangu amekuwa akisumbuliwa na maradhi ya kansa kwa kipindi kirefu na mauti yamemfika akiwa katika hospitali ya Lugalo jijini Dar. 
 
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Jordan Rugimbana taratibu za mazishi zinaandaliwa na taarifa kamili itatolewa hapo baadaye.Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi. AMINA

No comments:

Post a Comment