Pages

Wednesday, September 26, 2012

NYIMBO ZA "AFANDE SELE" ZA PIGWA STOP KUCHEZWA RADIONI MOROGORO

Ni baada ya kama miaka kadhaa kupita sasa kufanyika kitendo kama hicho katika radio moja mjini morogoro kusimamisha kupiga nyimbo za msanii Afande Sele  kituoni hapo.
Ni baada ya Chuma blog kumtafuta msanii huyo na kuamuwa kufunguka kwa kusema kuwa ni kweli amesikia jambo kama hilo kuwa azitakiwi kupigwa nyimbo zake tena katika radio hiyo na hata zile alizoshilikiana na wasanii wengine.Afande alizidi kufunguka kwa kusema kuwa yeye pia anashanga sana kwa jambo hilo.Akiwa kama yeye ni mkazi wa mkoa huo na kuona hata chombo cha nyumbani kina fanya mambo tofauti.

Ila ilinibidi kuzidi kumuuliza kwa kumbana kunipa ukweli wa mambo kama kuna tatizo lingine zaidi ?Alisema kuwa jambo ili lishatokea apo nyuma na tukawa tumeyamaliza kwa kuombana  "Msamaha" katika uongozi wa kituo hicho,Ila kwa mwaka huu nashanga kuona jambo hilo tena.
Alizidi kufunguka kwa kusema yeye sio mbunge na wala atalajii kuwa mbunge wa morogoro,ila wananchi ndio wanamlazimisha kugombea.Cha zaidi aliniakikishia kuwa yeye hana chama chochote cha siasa na anavipenda vote. "Afande sele" alisema
 HABARI KWA HISANI YA CHUMA BLOG

No comments:

Post a Comment