Wiki iliyopita picha za muigizaji wa filamu nchini, Aunt Ezekiel
akifunga ndoa zilisambaa kwa kasi kwenye mtandao na kuzua maswali mengi
kama iwapo amefunga ndoa kweli ama ni usanii tu. Wengi waliamini kuwa
amefunga ndoa na wengi pia walikuwa na mashaka.
Waliokuwa na mashaka
walihisi si kweli kutokana na sababu zifuatazo.

1. Aunt Ezekiel alikuwa akiendelea kukusanya michango ya harusi iweje aamue kufunga ndoa wakati bado anachangisha?
2. Kwanini harusi yake isihudhuriwe na watu wake wa karibu hata kama ni ya kiislamu? (kutokana na picha hizo)
3. Aliwahi kuhojiwa na kudai kuwa angefunga ndoa mwezi November
Lakini ukweli kuwa picha hizo zilimaanisha kuwa
tayari amefunga ndoa. Lakini kuna sababu za harusi yake kuwa hivyo.
“Ni mchumba wangu na hakika yeye ndiye mwenye maamuzi nikaamua
nifanye hivyo,” ameiambia ‘Movie Leo’ ya Clouds FM.“Naweza sema bado
yaani siko sawa mpaka nihakikishe hivyo vitu vyote vimeenda vimepita
salama manake unajua shughuli yoyote hata kama ndogo lakini lazima
unajua yaani unakaa ni pressure yaani sijui itakuaje sijui itakuwa
vipi?
Kwahiyo naweza kusema kwasababu ni mwanzo kwahiyo bado kiukweli
naona yaani huko mbele kutakuaje.”Kutokana na kufanya mchakato wake ‘kiflashback’ yaani kuanza na hatua
ya mwisho ya harusi na kurudi nyuma, muigizaji huyo pia ameelezea jinsi
Kitchen Party za Send-off zitakavyokuwa, “nataka nifanye vitu vya
tofauti na kila kitu nataka kiwe tofauti na vile watu ambavyo wamezoea
kuviona au wamewahi kwenda , kwahiyo mwisho wa siku nikisema niseme
itakuaje, itakuwa hivi itakuwa hivi naweza nikawa nimezusha ugomvi.”
And by the way sasa jina lake ni Rahma baada ya kubadilisha dini na kuwa muislamu.
No comments:
Post a Comment