Pages

Friday, October 26, 2012

KICHANGA CHAOKOTWA KIKIWA KIMETUPWA CHINI YA MLIMA KIVES.

Hizi ni picha tulizozipata kwenye mtandao wa Jamii Forum zikiwa na maelezo: MAJONZI, HUZUNI, NA SIMANZI ZIMETAWALA LEO MAENEO YA KIJENGE JUU KATA YA KIMANDOLU ILIYOKO MKOANI ARUSHA BAADA YA KITOTO KICHANGA KUKUTWA KIMETUPWA CHINI YA MLIMA KIVESI. 

Baadhi ya wananchi waliojitokeza kuuangalia mwili wa kichanga hicho.Hakuna maelezo kuwa kichanga hicho kinekutwa hai kwakuwa mtu aliyeweka picha ametumia maneno kama ‘mwili’ wa mtoto huyo kumaanisha kuwa hakuwa hai. .

Mtoto mwenye umri wa siku moja wa jinsia ya kike akiwa amewekwa kwenye ndoo na kutupwa

Afisa wa polisi akiuchukua mwili wa mtoto huyo uliofungwa na kanga na kutolewa na msamaria mwema muda mfupi baada ya kutaarifiwa kuhusu tukio hilo

No comments:

Post a Comment