Pages

Friday, October 19, 2012

ROSE CHITALA AVAMIWA NA JAMBAZI, AJERUHIWA MKONO.

MWANAUME anayedhaniwa ni jambazi amemvamia na kumjeruhi Mtangazaji wa Radio Times FM ya jijini Dar, Rose Bernard Chitala na kumjeruhi mkono kwa kutumia panga. Tukio hilo lilijiri usiku wa saa tano, Oktoba 14, mwaka huu maeneo ya Legho, Shekilango, Ubungo, Dar wakati mtangazaji huyo akijiandaa kwenda kwake, Sinza Madukani.

Mtangazaji Rose Chitala akiwa na huzuni baada ya tukio la kuvamiwa na kujeruhiwa na mwanaume anayedhaniwa kuwa ni jambazi.

 Akizungumza nyumbani kwake akiwa katika maumivu makali, Rose alisema siku hiyo alikuwa na kikao na marafiki zake watatu kwenye Uwanja wa Sanaa, Legho.“Baada ya kumaliza kikao, nikawa naondoka, kufika kituoni, gari moja aina ya Toyota Cresta lenye namba za usajili BWM 571 lilifika jirani yangu na kutaka kunigonga, mara akashuka mwanaume na kunivamia kisha akaanza kunipiga.
 
“Nilipomuuliza ni nini kinaendelea na anataka nini kwangu, akaenda nyuma ya gari na kufungua buti, akatoa panga ambalo alinirushia, lakini bahati nzuri nilijikinga na pochi niliyokuwa nimeshika. Nilipolizuia lile panga, liliteleza na kunikata mkono na kidole kama hivi,” alisema Rose.

Akaendelea kueleza kuwa timbwili zito liliibuka eneo la tukio ambapo watu walianza kujaa huku wakimpigia kelele za jambazi mtu huyo, kuona hivyo, aliingia kwenye gari na kuondoka kwa kasi.
Hata hivyo, alisema mmoja wa marafiki zake hao, alikodi bodaboda na kulikimbiza gari hilo na ndipo alipofanikiwa kulisoma namba zake za usajili.Hata hivyo, Rose alikwenda kiripoti Kituo cha Polisi Urafiki Ubungo, Dar ambapo aliandikisha maelezo yenye Kumbukumbu No. URP/RB/8105/12; SHAMBULIO na gari hilo linasakwa usiku na mchana.

No comments:

Post a Comment