Pages

Monday, October 1, 2012

WAFANYAKAZI WA BARCLAYS WAFANYA BONANZA LA MICHEZO

Wacheza  mpira kikapu  wa Benki ya Barclays Tanzania wakichuana ili kumpata mshindi  wakati wa bonanza la michezo la kila mwaka la benki hiyo katika Viwanja vya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki.
Baadhi ya wafanyakazi wa benki ya Barclays Tanzania, wakishindana katika mchezo wa kuvuta kamba katika bonanza la michezo la kila mwaka la benki hiyo, katika Viwanja vya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki.
Wasakata kabumbu wa Benki ya Barclays Tanzania, Paul Abduel (kushoto) na Stanslaus Mkondya (kulia) wakigombea mpira katika bonanza la michezo la kila mwaka la benki hiyo, katika Viwanja vya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki.
Baadhi ya wafanyakazi wa Barclays wakiselebuka katika bonanza la Siku ya Michezo katika Viwanja vya UDSM jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Barclays Tanzania, Kihara Maina (katikati) akipozi kwa picha na timu iliyoibuka kidedea katika mchezo wa soka wakati  bonanza la Siku ya Michezo katika Viwanja vya UDSM jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Mawasiliano wa Benki ya Barclays Tanzania, Tunu Kavishe akizungumza wakati wa bonanza hilo ambapo wafanyakazi hao walishiriki michezo ya kuvuta kamba, kabumbu, wavu, kikapu na kusakata dansi. 

No comments:

Post a Comment