Pages

Tuesday, November 27, 2012

Amuua mama yake kwa mateke na ngumi.

MKAZI wa Swaya, jijini Mbeya, Ndele Julius, anatafutwa na polisi kwa tuhuma za kumuua mama yake mzazi kwa kumpiga mateke na ngumi.

Taarifa ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Diwani Athuman, iliyotumwa kwa waandishi wa habari jana, ilieleza kuwa tukio hilo lilitokea Novemba 25, mwaka huu, eneo la Swaya.
Taarifa hiyo ilimtaja mwanamke huyo aliyeuawa kuwa ni Sinjembele Julius (62), aliyekuwa mkulima.

“Chanzo cha kifo hicho ni mtuhumiwa kuwa na ugomvi na kijana mwenzake ndipo mama yake alipokwenda kuamulia ugomvi na kugeukwa na mwanaye kisha kuanza kushambuliwa,” ilieleza sehemu ya taarifa hiyo.Ilielezwa kuwa baada ya mauaji hayo, mtuhumiwa huyo alikimbia, hivyo Jeshi la Polisi linatoa wito kwa mtu au watu wenye taarifa juu ya mahali alipo mtuhumiwa, ili akamatwe au ajisalimishe mwenyewe. Habari na Gordon Kalulunga, Mbeya

No comments:

Post a Comment