Pages

Sunday, November 25, 2012

Chelsea 0 Man City 0 …Benitez humwambii kitu kwa Abramovich.

LONDON, ENGLAND
KOCHA wa muda wa Chelsea, Rafa Benitez amekaribishwa kwa sare ya bila bila dhidi ya Manchester City katika dimba la Stamford Bridge muda mfupi uliopita.
Benitez alilakiwa na mabango mengi yaliyomdhihaki wakati mchezo unaendelea, mengi kati ya mabango hayo yakisema “Benitez Out” huku mengine yakimsifia kocha aliyetimuliwa Roberto Di Mateo.
Hata hivyo Kocha huyo akizungumza kabla ya mechi hiyo, alimwagia sifa nyingi mmiliki wa Chelsea Roman Abromovich.
Benitez alisema anaamini Roman Abramovich ni "mtu mzuri", baada ya kukutana naye kwa mara ya kwanza Alhamisi.
Benitez alitumia "saa mbili au tatu" akiwa na mmiliki huyo wa Chelsea Alhamisi jioni, baada ya kutangazwa rasmi kuwa kocha mpya wa klabu katika mkutano na waandishi mapema siku hiyo.
Kocha huyo anaamini kuwa ataweza kufanya kazi vizuri na mmiliki huyo baada ya mazungumzo yenye tija.
Abramovich ana sifa ya ​​kutovumilia kushindwa - moja ya ushaidi wa hilo ikiwa hatua yake ya hivi karibuni ya kumtupia virago Roberto Di Matteo - lakini Benitez anaamini kwamba matakwa ya Abramovich hayana tofauti na ya wamiliki na wenyeviti wake wengi wa zamani.
"Nina miaka 26 katika uongozi wa klabu na naweza kuhakikisha kuwa nimekuwa na wamiliki wengi tofauti na wenyeviti," Benitez alisema. "Kama una ujasiri wewe binafsi na unaweza kujieleza mwenyewe, kila mtu anaweza kuelewa.
"Maoni yangu kuhusu yeye (Abramovich), ni kwamba ni mtu mzuri. Unaweza kuzungumza nae. Anaelewa. "
Mhispania huyo anasaema kuwa, anamuelewa vizuri Abramovich, kwamba ni mtu ambaye anataka maamuzi ya kutenda zaidi kwa wafanyakazi wake badala ya kuweka mbele dhana na hisia.
"Yeye anapenda kuona ukiwa na wazo wazi: 'Nadhani ni wazi' kwa sababu ya hili au lile, au hili haliwezekani kwa sababu ya hili au lile'," Benitez aliongeza.
"Wakati tukipata chakula cha jioni, ilivutia wakati tulipokuwa tukizungumza juu ya kila kitu. Anajua mawazo yangu kuhusu (staili ya uchezaji ya) kukaba nafasi, na yeye anajua kwa nini napendelea hili.
"Sote tulizungumza. Kawaida mimi huzungumza sana. Kipaumbele cha mmiliki ni kama mimi ni meneja mzuri, kocha mzuri, kama wachezaji wananielewa, kama tutaweza kuwa timu ya kushinda. Yeye alikuwa wazi sana na hili."
Matokeo ya mechi zingine za leo ni Tottenham 3 West Ham 1, Southampton 2 Newcastle o  huku Liverpool ikipata sare ya 0-0 kwa Swansea.
Via SALUTI 5 - www.saluti5.com

No comments:

Post a Comment