Pages

Friday, November 23, 2012

HILI NI DONGO LA WAZI KWA KINA WEMA SEPETU …KAPTURADO ASEMA MSITUHARIBIE BONGO MOVIE, RUDINI KWA KINA LUNDENGA.

MWIGIZAJI na mtayarishaji wa filamu Swahiliwood, Simon Mwapagata ‘Kapturado’ amewashauri wasanii walioingia katika tasnia ya filamu wakitokea katika tasnia ya ulimbwende warudi huko baada wao kuwa ni chanzo cha kashifa katika tasnia ya filamu Bongo Rado anasema kuwa walimbende hao ndio wanaovuma kwa matukio ngono na mavazi ya kujifedhehesha.
“Mimi nikiwa kama mwanzilishi ya Bongo Movie Unity nina uchungu sana na tabia ya hawa akina dada waliovamia tasnia ya filamu wakitokea katika fani ya urembo wamekuja kutuharibia tasnia ya filamu kwa kufanya matukio ya ajabu ajabu, ngono mara mavazi ya nusu uchi hiyo siyo filamu ninawashauri warudi kwa Lundenga ndio anawezana nao,”anasema Rado kwa uchungu.
Rado amedai kuwa sababu kubwa ya kuanzishwa kwa kundi hilo ililenga kubororesha tasnia ya filamu na si sehemu ya baadhi ya wasanii kuja kujiuza au kuvaa nusu uchi katika majukwaa kama ambavyo imekuwa ikifanyika madongo yaliwalenga wasanii ambao ambao ni gumzo kwa kashifa Bongo Aunty Ezekiel na Wema Sepetu ambao wote waliingia katika tasnia ya filamu wakitokea umiss.
Chanzo: habari hii ni kwa hisani ya www.filamucentral.co.tz

No comments:

Post a Comment