Pages

Wednesday, November 28, 2012

KABURI LA KANUMBA LAGEUKA KIMBILIO LA WASANII.

JANA mara baada ya kumalizika kwa mazishi ya John Stephano Maganga, baadhi ya wasanii wa filamu walikwenda ng’ambo ya pili ya makaburi kulifuata kaburi la The Great Steven Kanumba.
Katika hali iliyovuta macho ya wengi, kaburi la Kanumba ambalo liko umbali wa kama mita 100 kutoka kaburi la John Maganga, lilikuwa kimbilio la wasanii wengi huku wengine wakisema wanakwenda ‘kuhiji’ kwenye kaburi la The Great.
Miongoni mwa wasanii waliobahatika kupita kwenye kamera ya saluti5 ni pamoja na Mainda, Mzee Chilo, Pendo na Top Model wa Miss Tanzania miaka kadhaa iliyopita, Rashida Wanjara.Chanzo cha habari na Saluti5

No comments:

Post a Comment