Pages

Friday, November 9, 2012

MAPACHA WATATU WAJA NA STAILI YA KUGANDANA.

BENDI ya Mapacha Watatu “Wakali wa Town” wameibuka na staili mpya ya kugandana ambayo itatambulishwa leo katika ukumbi wa Business Park Kijitonyama.
Mmoja wa wakurugenzi wa kundi hilo, Khalid Chokoraa aliiambia www.saluti5.com kuwa hicho ni kitu kipya ambacho ndani yake kutakuwa na rap kali ya kunasia a.k.a kugandana.
“Watu wanaweza wakadhani staili hii inahusiana na kile kilichotokea leo (jana) kule Temeke, jibu kamili watalipata Business Park” alisema Chokoraa.
Chokoraa amesema katika onyesho hilo lililopewa jina na Full kugandana, Mapacha Watatu watasindikizwa na kundi la Baikoko. “Itapendeza sana kama utakuja na patna wako” aliongeza Chokoraa
Mapacha Watatu “Wakali wa Town”.
CHANZO NI KUTOKA SALUTI5 (www.saluti5.com).

No comments:

Post a Comment