Pages

Friday, November 23, 2012

RONALDO ATOA KIATU CHAKE CHA DHAHABU KIUZWE MAPATO YAENDA KUSAIDIA WATOTO GAZA.

Vyombo vya habari vingi barani ulaya vimeripoti kwamba Cristiano Ronaldo ametoa msaada wa €1.5 million kwa watoto wa mji wa  Gaza. Lakini ukweli ni kwamba msaada huo umetoka kwa Real Madrid foundation ambao walichangisha kiasi hicho kutokana na mauzo kiatu cha dhahabu alichoshinda Ronaldo msimu wa 2010-11.

Mwaka jana Mreno huyo aliuza viatu vyake vingi vya michezo na fedha zilizopatikana alizitoa kwa Real Madrid Foundation ambao wakazipeleka kwa shule za watoto huko Gaza.Real Madrid Foundation imesaidia kujenga shule 167 katika nchi 66 tofauti.

No comments:

Post a Comment