Pages

Wednesday, November 7, 2012

Wataalamu IT wajadili wizi wa mitandao.


WATAALAMU wa masuala ya mtandao wa ndani na nje ya nchi (IT), wamekutana jijini Dar es Salaam kuangalia njia za kudhibiti wizi kwa njia ya mitandao.
Mbali ya hilo, wataalamu hao wameangalia pia namna ya kulinda na kutunza taarifa wanazopata katika kampuni mbalimbali nchini.
Akizungumza baada ya ufunguzi wa warsha hiyo ya siku moja, Rais wa Ukaguzi kutoka taasisi inayohusika na mitandao Tanzania (ISACA), Boniface Kanemba, alikiri kuwepo kwa tatizo katika tasnia hiyo.


Aliongeza kuwa, awali Watanzania walidhani matukio mengi ya wizi yanasababishwa na utumiaji wa silaha kama kujilinda, lakini sasa wezi hao wanakwenda na wakati, wakibuni njia mbadala ya mitandao kufanikisha malengo.
“Kutokana na ongezeko la matumizi ya mitandao kwa njia ya benki, kampuni na hata simu, kuna haja ya kukabiliana na tatizo hili mapema kwa sababu limeonekana wazi kushamiri tofauti na awali.

“Tumekutana na wenzetu kutoka nchi za Norway, Lithuania, wakiwemo wa sekta mbalimbali nchini, kuangalia namna ya kuwalinda wateja pindi wanapokumbwa na dhoruba hiyo,” alisema.
Mwakilishi kutoka Norway ambaye ni Mkurugenzi Mwendeshaji wa Kampuni ya Quintex Financial Services of Dar es Salaam, Ntinabo Rwegasira, alisema vyombo vya dola kama Jeshi la Polisi na uhamiaji vina nafasi kubwa ya kuhakiki au kudhibiti kundi hilo la wizi lisiendelee endapo watafanya kazi zao kwa makini.

No comments:

Post a Comment