Pages

Friday, December 28, 2012

BARAZA LA WAZEE SIMBA LAPIGA MKWARA MKUTANO WA JUMAPILI

KUFUATIA mkutano ulioitishwa na baadhi wa wanachama wa Simba Jumapili hii, Baraza la Wazee wa klabu hiyo ya mtaa wa Msimbazi, limewataka wanachama hao kutoitisha mkutano huo kwa vile mkutano huo si halali.
Kaimu Katibu Mkuu wa Baraza hilo, Zuberi Mpacha, alisema jana kuwa si kweli kuwa wanachama wakifika 500 wanakuwa na uwezo wa kuitisha mkutano.
Zuberi alisema kuwa mkutano bila ya ridhaa ya uongozi si halali hivyo kufanya hivi itakuwa kinyume na katiba ya Simba.
Akinukuu baadhi ya vifungu vya katiba ya Simba, Zuberi alisema kifungu cha 22 kinakataza kuwepo kwa mkutano bila ya ridhaa ya viongozi.“Baraza la Wazee tunasema mkutano huo si halali kabisa, kama kuna matatizo ndani ya uongozi kuna sehemu ya kusuluhisha na si kutumia mikutano ambayo si halali” alisema Mpacha.
Baadhi ya wanachama wameitisha mkutano wa dharura kupinga uongozi wa klabu kufutia kufanya vibaya katika mzunguko wa kwanza wa Ligi kuu Tanzania Bara.Via saluti5.

No comments:

Post a Comment