Pages

Monday, December 31, 2012

HATIMAYE FILAMU YA HARAKATI YATINGA SOKONI

ILE filamu iliyotokea kuzua gumzo kabla haijatoka, inayokwenda kwa jina la ‘Harakati’, imetinga sokoni leo ambako inasambazwa na Kampuni ya Steps Entertainment.
Filamu hiyo inashirikisha nyota kadhaa wa filamu za Kibongo, akiwamo Rashid Waziri, Fikiri Salum, Jenifer Raymond na Mshindo Jumanne.
Taarifa kutoka ndani ya Kampuni ya SSG Distributors iliyotengeneza muvi hiyo, zinasema kuwa, kuanzia sasa, itapatikana nchi nzima kwenye DVD pamoja na VCD.
“Harakati ni miongoni mwa muvi kali kupita kawaida za Kampuni yetu, ambayo tunaamini itafanikiwa kuteka vilivyo nafsi za mashabiki wetu,” ilisema taarifa hiyo.

No comments:

Post a Comment