Pages

Thursday, December 27, 2012

MANCHESTER UNITED UGONJWA WA MOYO, YAFUFUKA MARA 3 KWA NEWCASTLE, LIVERPOOL HAINA JIPYA.


KWA wapenzi wa Manchester United hali ilikuwa ni ya kihoro katika mchezo wa Ligi kuu ya Uingereza dhidi ya Newcastle uliochezwa kwenye uwanja wa Old Trafford.
Manchester United ililazimika kusawazisha mara 3 na hatimaye kupata bao la nne dakika ya tisini lililoipa ushindi wa mbinde wa 4-3.
Hernendes akipiga bao la nne na la ushindi
Imekuwa ni kama jadi sasa kwa United kutoka nyuma na kuibuka na ushindi, hali ambayo imekuwa ikiwaweka roho juu mashabiki wake katika kila mchezo.
Newcastle walianza kuongoza dakika ya 4 ya mchezo kwa goli la James Perch, John Evans akasawazisha dakika ya 25.

NET GAINS ... Perch breaks the deadlock
Newcastle wanaadika bao la kwanza
JONNY BE GOOD ... Evans wheels away after making it 1-1
John Evans anaiswazishia Manchester United
Dakika tatu baadae, juhudi za Evans zikawa ni kama kazi bure, dakika 28 akaipa Newcastle bao la zawadi pale alipojifunga katika juhudi zake za kuokoa, goli ambalo lilizua utata mkubwa miongoni mwa waamuzi.
OH EVANS ... United defender goes from hero to zero
Evans anajifunga, bao la pili kwa Newcastle
CONTROVERSY ... assistant ref Jake Collin initially rules out Evans' own goal
Mshika kibendera anasema sio goli
CHEER WE GO ... Toon go wild as goal is given
Refarii anasema ni goli, Newcastle wanashangilia 2-1
Kipindi cha pili dakika ya 58 Evra akaisawazishia Manchester United, lakini Newcaslte wakawa mbele tena dakika ya 68 kwa bao safi la Cisse.
Robin Van Persie akairudisha mchezoni Manchester United kwa goli la dakika ya 71, hili likiwa ni goli lake la 13 kwa United katika Ligi kuu ya Uingereza tangu alipojiunga nayo mwanzoni mwa msimu huu.
Shujaa wa mchezo akawa ni Javier Hernandes pale alipoitumia vema pasi ya kiungo Michael Carrick na kufunga bao maridadi dakika ya 9o.
Katika mchezo mwingine, Liverpool ilichapwa na Stoke City 3-1, huku Totenham Spurs ikivuna ushindi wa 4-0 kwa Aston Villa.
Matokeo ya mechi zote zilizochezwa jana ni kama ifuatavyo:
Everton 2 – 1 Wigan
Fulham 1 – 1 Southampton
Manchester United 4 – 3 Newcastle United
Norwich 0 – 1 Chelsea
Reading 0 – 0 Swansea
Sunderland 1 - 0 Manchester City
Queens Park Rangers 1 – 2 West Bromwich Albion
Aston Villa 0 – 4 Tottenham
Stoke City 3 – 1 Liverpool

No comments:

Post a Comment