Pages

Saturday, December 29, 2012

Wahamiaja haramu 18 wafariki Misri

Balozi wa Somalia nchini Libya Bwana Abdikani Mohamed Waeys amesema ana taarifa ya vifo vya raia 18 vilivyotokea kutokana na ajali ya lori nchini Libya.Wasomali hao wanaotajwa kuwa wahamiaji haramu, 23 wameripotiwa kujeruhiwa huku wengine wakiwa katika hali mbaya.
 Wahamiaji haramu
                                          Wahamiaji haramu wakijaribu kuvuka baharini
Balozi Abdikani amesema lori hilo lililokuwa limebeba mifuko ya saruji walimokuwa wamejificha Wasomali hao, lilipinduka na kusababisha vifo, na kusema idadi yao walikuwa 120 wakiwemo wanaume na wanawake wote wakiwa ni Wasomali.Katika miaka ya hivi karibuni idadi ya wahamiaji haramu ambao wamefariki wakijaribu kuvuka baharini imeongezeka.

No comments:

Post a Comment