Pages

Wednesday, December 26, 2012

WOLPER, BABY CANDY POZI TATA

Na Mwandishi Wetu(Habari na www.globalpublishers.info )
PICHA za mastaa wa Kibongo Jacqueline Wolper Masawe na Baby Candy zimenaswa katika mtandao wa BBM na kuzua utata kutokana na pozi lao, Risasi Mchanganyiko linakumegea.
 
Jacqueline Wolper Masawe na Baby Candy katika pozi la kimahaba.
Wawili hao ambao wote wana majina katika tasnia za filamu na muziki wamepiga picha na kukaa katika pozi tata kiasi cha kuacha maswali kwa wadau wa fani zao.
Katika picha hiyo, Wolpler anaonekana akiwa amesimama mbele ya Baby Candy na kurudisha mkono wake nyuma huku akiingiza kidole mdomoni mwa msichana mwenzake huyo (angali picha uk 16).
Mashabiki wa mastaa hao walipoiona picha hiyo iliyotupiwa kwenye mtandao huo wa BBM walisema kuwa pozi hilo ni la kimahaba na si zuri kwa watoto wa kike.

 
Jacqueline Wolper Masawe.
“Jamani sasa ndiyo nini? Hili pozi la Wolper na Baby Candy linaashiria nini wakati  wote ni wasichana?” alihoji mmoja wadau wa burudani aliyeiona picha hiyo.
Hata hivyo, pamoja na idadi kubwa ya watu kuwasema vibaya, lakini baadhi waliwatetea kwa kusema kuwa pozi lao lilikuwa ni la kawaida sana.
Hali hiyo ya kuwatetea wawili hao, ilizua ubishi kwa baadhi ya watu waliokuwa wakichangia mada hiyo kwa kusema kuwa picha  hiyo haifai katika jamii yetu.
“Hata kama ni marafiki kwa kupiga picha hiyo wamefika mbali kwani mambo ya kuumana vidole hufanywa na makahaba zaidi,” alisema  mdau mwingine.

No comments:

Post a Comment