Pages

Sunday, January 27, 2013

Akaunti ya Twitter ya kundi la wapiganaji wa kiisilamu la al-Shabab , imefungwa


Akaunti ya Twitter ya kundi la wapiganaji wa kiisilamu la al-Shabab , imefungwa kwa sasa baada ya kundi hilo kuitumia kwa kutoa vitisho vya kuwaua mateka wawili wa Kenya wanaowazuilia.
Al-Shabab ilifungua akaunti hiyo mwezi Disemba mwaka 2011, baada ya majeshi ya Kenya kuingia Somalia kupambana na wanamgambo hao.
Mapema mwezi huu, kundi hilo lilitumia Twitter kutangaza itamuua jasusi wa Ufaransa ambaye walikuwa wamemzuilia na hatua iliyofuata ilikuwa ya kutekeleza mauaji hayo.
Twitter hata hivyo ilikataa kuzungumzia hatua yake ya kuibana akaunti hiyo lakini ikasema kuwa vitisho vya kufanya vitendo kama vya mauaji ni marufuku kuvitangaza kupitia mtandao huo.Siku ya Jumatano, al-Shabab ilipeperusha kanda ya video kwenye ukurasa wake kuhusu mateka hao wa Kenya wanaozuiliwa Somalia, na kuiambia serikali ya Kenya kuwa maisha ya wawili hao yamo hatarini ikiwa waisilamu wote wanaozuiliwa kwa tuhuma za vitendo vya kigaidi hawataachiliwa.
Al-Shabab, ambao wana uhusiano na kundi la al-Qaeda, walisema kkuwa walimuua jasusi wa Ufarans Denis Allex kulipiza kisasi kwa operesheni ya makombando wa Ufaransa kumuokoa iliyotibuka.
Serikali ya Ufaransa ilisema kuwa inaamini bwana Allex aliuawa wakati wa operesheni hiyo, wiki mbili zilizopita, katika tukio ambalo makomando wa Ufaransa pia waliuawa.
Allex alikamatwa mwezi Julai mwaka 2009.
Jeshi la Kenya lilifanikiwa kuondoa Al-Shabab kutoka miji muhimu ya nchi hiyo katika kipindi cha miezi kumi na minane iliyopita, inghawa wangali wanadhibiti Kusini na maeneo ya kati mwa Somalia.
CHANZO: BBC SWAHILI

No comments:

Post a Comment