Pages

Monday, January 28, 2013

Misri haikutumia silaha dhidi ya waandamanaji

Msemaji rasmi wa vikosi vya jeshi la ulinzi la Misri amekadhibisha habari iliyotangazwa na baadhi ya vyombo vya habari kuwa jeshi la nchi hiyo limetumia silaha kuwakandamiza wafanya maandamano nchini humo. 
 Misri haikutumia silaha dhidi ya waandamanaji

Ahmad Muhammad Ali amekanusha habari iliyotangazwa na baadhi ya vyombo vya habari kwamba jeshi la Misri limewafyatulia risasi waandamanaji huko katika mji wa Port Said na kuwauwa raia wengi miongoni mwao. Msemaji wa vikosi vya jeshi la ulinzi la Misri amesisitiza kwamba hakuna raia yoyote wa Misri aliyeuliwa kwa kufyatuliwa risasi. Amevitaka vyombo vya habari kuacha kutangaza habari zisizo sahihi kuhusiana na yale yanayojiri huko Port Said. Watu 31 wameuawa na wengine 445 kujeruhiwa katika mapigano yaliyotokea juzi Ijumaa huko Cairo na katika miji mingine ya Misri.

No comments:

Post a Comment