Pages

Thursday, January 31, 2013

Mshiriki Maisha Plus 2012 Rashid Ndunduke afariki dunia

ALIYEKUWA mshiriki wa shindano la Maisha Plus 2012, Rashid Ndunduke, amefariki dunia kijijini kwao juzi baada ya kuvamiwa na kiboko.
Rashid ambaye kwenye shindano hilo la Maisha Plus alikuwa akiwakilisha Mkoa wa Lindi, alikuwa kivutio kwa watazamaji wengi, hasa kwa mambo mbalimbali aliyokuwa akifanya ndani ya kijiji hicho, ikiwamo kuonesha maisha halisia.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana na kaka wa marehemu, Hassan Ndunduke, mdogo wake alikutwa na mauti akiwa anavua samaki, ghafla kiboko alimvamia na kumjeruhi.
Hassan alisema licha ya juhudi za hospitali ya jirani huko kijijini kwao Njinjo kuokoa maisha yake zilishindikana.

Marehemu alijiunga Maisha Plus kama mmoja wa wawakilishi wa Mkoa wa LindiAkiwa kijijini Maisha Plus, alifahamika kwa wengi kama Nanjilinji, Master Key au Baba Sampo.
Shughuli alizozifanya Maisha Plus ni pamoja na kuuza duka, uchongaji na kuna wakati aliwahi kuongoza kwa kuwa na fedha nyingi zaidi ikilinganishwa na wanakijiji wenzake, sambamba na uhodari wa kukwea miti mirefu

No comments:

Post a Comment