Pages

Wednesday, January 23, 2013

Yanga yailabua tena Black Leopards 2-1 huko CCM Kirumba, Mwanza

Timu ya Young Africans Sports Club imeendeleza wimbi lake la ushindi baada ya kuichapa timu ya Black Leopard ya Afrika Kusini mabao 2-1 katika mchezo wa kirafiki uliofanyika leo jioni katika Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.
 
                        Mashabiki wakiwa kwenye mstari kwa ajili ya kuingia uwanjani.
Kikosi cha kocha mholanzi Ernest Brandts kiliuanza mchezo kwa kasi kwa lengo la kusaka bao la mapema, kwani timu ya Black Leopard nayo leo iliingia ikiwa na dhamira ya kupata ushindi na kuondoa hali ya kufungwa mara ya pili na Young Africans.
 
                                               Kikosi cha timu ya Black Leopards.
Iliwachukua watoto wa jangwani dakika 3 tu kujipatia bao la kwanza lililofungwa na mshambuliaji Said Bahanuzi kwa kichwa akimalizia mpira uliopigwa na Kabange Twite na kugonga mtambaa wa panya kabla ya kumkuta mfungaji Bahanuzi aliyeukwamisha mpira wavuni.
 
Black leopard iliibadilika na kucheza kwa kasi ili kusaka bao la kusawazisha na katika dakika ya 12, mshambuliaji wa Black Leopard Joshua Obaje aliipatia timu yake bao la kusawazisha kufuatia uzembe wa walinzi wa Yanga waliozembea kumkaba mfungaji huyo aliyepiga shuti kali na mpira kutinga wavuni.
Timu zote zilicheza soka la kushambuliana kwa zamu na nusra Bahanuzi tena aipatie Young Africans bao la pili lakini umakini wa mlinda mlango Postentt Omony aliweza kuokoa mchomo huo na kutoka nje kuwa kona ambayo haikuzaa matunda.
 
Mpaka dakika 45 za kipindi cha kwanza Young Africans 1- 1.
 
Kipindi cha pili kilianza kwa Young Africans kufanya mabadiliko ambapo kocha Brandts aliwatoa Kabange Twite, Nurdin Bakari, David Luhende, Said Bahanuzi, Hamis Kiiza na nafasi zao kuchukuliwa na Haruna Niyonzima, Athumani Idd, Jerson Tegete, Frank Domayo na Didier Kavumbagu.
 
Young Africans ilibadilika sana uchezaji na hasa eneo la kiungo ambapo Frank Domayo, Haruna Niyonzima na Athumani Idd waliweza kuwafunika kabisa viungo wa timu ya Black Leopard.
 
Dakika ya 53 Jerson Tegete aliipatia Young Africans bao la pili kwa mkwaju wa penati kufuatia mlinzi wa Black Leopard Vicent Mabwisela kumchezea ndivyo sivyo mshambuliaji wa Young Africans Didier Kavumbagu na Tegete kuukwamisha mpira huo wavuni.
 
Yanga iliendelea kulishambulia lango la Black Leopard kwa dakika zote za kipindi za kipindi cha pili na kama washambuliaji wake Didier Kavumbagu, Jerson Tegete na Saimon Msuva wangekua makini timu ingeibuka na ushindi wa mabao mengi.
 
Black Leopard iliendelea kucheza kwa nguvu kusaka bao la kusawazisha lakini umakini wa walinzi Yanga ilikuwa kikwazo kwao kuweza kupata bao la kusawazisha.

Dakika ya 89, Kelvin Yondani alitolewa nje kwa kadi nyekundu na mwamuzi Alex Mahagi baada ya kumchezimu ya ea madhambi mshambuliaji wa timu ya Black Leopard.
 
Golikipa wa timu ya Black Leopards,Posnett Omony akisota kuokoa mpira uliotinga wavuni kutoka kwa mchezaji wa timu ya Yanga,Jerry Tegete kwa njia ya penati mnamo dakika ya 54.Timu ya Yanga imeibuka kifua mbele mpaka dakika 90kwa kuinyuka goli 2-1 timu ya Black Leopards kwenye mchezo wao wa marudiano wa kirafiki uliofanyika kwenye uwanja wa CCM-Kirumba jijini Mwanza.
Mpaka mwisho wa mchezo Young Africans 2- 1 Black Leopard.
 
Kocha mkuu wa Yanga Ernest Brndts amesema anashukuru timu yake kwa kupata ushindi huo wa leo, kwani timu ya Black Leopard ni timu nzuri,naleo ilingia kucheza kwa nguvu ili ipate ushindi na kufuta uteja dhidi ya Yanga lakini mwisho wa siku vijana wangu walikuwa ni bora zaidi ndio maana wameibuka na ushindi huo.
 
Kambi yetu ya mafunzo nchini Uturuki imetusaidia sana, wachezaji wanacheza kwa kujiamini wametulia  hawana presha ya mchezo, hali inayopelekea kucheza migongeano kwa uhakika na hii ni dalili tosha kuwa tupo tayari kwa mzunguko wa pili wa ligi kuu ya Vodacom alisema 'Brandts'
 
Naye kocha wa Black Leopard Abel Makhubele amesema timu yake leo ilicheza vizuri sana na kwa uelewano mkubwa, kwani hivi sasa wachezaji wake wamezoea hali ya hewa na mazingira, lengo letu likikuwa ni kuibuka na ushindi katika mchezo wa leo lakini makosa yaliyojitokeza kwa safu yetu ya ushindi ndiyo yaliyopelekea mchezo huu wa leo.
 
Hii ilikuwa ni mechi ya pili kucheza kwa Young Africans dhidi ya Black Leopard ambapo katika michezo yote Yanga imeibuka na ushindi wa mabao 3-2 katika mchezo wa kwanza jijini Dar es salaam na ushindi wa mabao 2-1 katika mchezo wa leo 
 
Young Africans itafanya mazoezi asubuhi katika Uwanja wa CCM Kirumba kabla ya kuanza safari ya kurejea jijini Dar es salaam majira ya mchana kwa shirika la ndege la Fast jest ambapo inatarajiwa kufika maira ya saa 12:30 jioni. 

Young Africans: 1.Ally Mustapha 'Barthez', 2.Mbuyu Twite, 3.Oscar Joshua, 4.Nadir Haroub'Cannavaro', 5.Kelvin Yondani, 6.Nurdin Bakari/Athuman Idd 'Chuji', 7.Saimon Msuva/Nizar Khalfani, 8.Kabange Twite/Frank Domayo, 9.Said Bahanuzi/Didier Kavumbagu, 10.Hamis Kiiza/Jerson Tegete, 11.David Luhende/Haruna Niyonzima

Black Leopard: 1.Posnett Omony, 2.Moses Kwena, 3.Thulani Ntishineila, 4.Vicent Mabsela, 5.Victor Kamhuka/Sizwe Sibiya, 6.Bafana Sibeko, 7.Tiyane Mabunda/Sphamandla Sibaiya, 8.Michael Nkabule/Raymond Monana, 9.Joshua Obaje/Mxolisi Gunede/, 10.Mondli MiyaThabo Mongalo, 11.David Zulu/Tommy Mandalazi

No comments:

Post a Comment