Pages

Sunday, February 24, 2013

Iringa: Ajali yametokea alfajiri, sababu ya ulevi wa pombe (?)

Picture
Picture
Picha na Meshack Maganga; Maelezo  na Francis Godwin (via blog)
Ajali  mbaya  imetokea  mjini Iringa majira ya saa kumi alfajiri ya leo,  eneo la Makosa ama CRDB ya  zamani kwenye barabara  kuu ya Iringa -Dodoma baada ya gari aina ya RAV 4 yenye namba za usajili T 319 AFL kuhama njia na  kuigonga  gari nyingine inayotumika kama taxi yenye namba  za usajili T 510 AYU iliyokuwa  ikiendeshwa na dereva Kevin Kaduma.

Ajali  hiyo  imetokea wakati  dereva  wa RAV4 hiyo akitokea maeneo ya mji  wa Iringa akielekea  mwelekeo ambao wakazi  wa mji wa Iringa wamekuwa  wakipata  starehe zao eneo la  Dragon Bar na Club  Twistas  kuendelea  kumalizia starehe za mwisho  wa wiki.Walioshuhudia ajali hiyo wamemeweleza Francis Godwin kuwa RAV 4 ilikuwa katika mwendo mkali mfano  wa gari  lililopo katika mashindano na  hivyo dereva  wake  kushindwa kukata kona ya mnara  wa Manispaa ya Iringa  na ndipo alipougonga ukuta  wa  barabara hiyo  kabla ya  kuhama na kuigonga taxi hiyo kwa  kuipanda  juu .

Wwalisema  kuwa  dereva  wa RAV 4 alikuwa anaonekana  kulewa pombe.

Dereva  aliyegongwa Kelvin Kaduma aliyekuwa akiendesha Taxi yenye namba  T 510 AYU akielezea chanzo  cha ajali  hiyo na jinsi ambavyo alivyonusurika kifo anasema aliiona RAV 4 ikija kwa mwendo wa kasi na ndipo alipoamua  kusimama na ghafla alijikuta akifunikwa na RAV 4 hiyo.

Alisema  kuwa  RAV 4 hiyo  iliruka  ukingo la  barabara  ambao  una michongoma na kujengwa kwa  sementi na kutua  juu ya gari lake na kushindwa  kuendelea na  safari. 

Anasema huenda kama siyo kusimama kwake,  basi  dereva wa RAV4 angekufa kwa  kugonga nyumba iliyopo jirani ambayo ina hoteli ya Hast Tast .

Hata  hivyo amesema hana mchumbuko  wowote na kuwa  dereva huyo wa RAV 4 kwa sasa anashikiliwa na  polisi baada ya  kushindwa  kukimbia kutokana na kulewa pombe.

No comments:

Post a Comment