Pages

Friday, February 1, 2013

Mchakato wa kuiboresha Dar ili lionekane kama miji mikubwa waja

SERIKALI inakamilisha mchakato wa kuboresha jiji la Dar es Salaam ili lionekane kama miji mikubwa ya mataifa mengine yaliyoendelea ifikapo mwaka 2032.

Mchakato wa kubadilisha jiji hilo unafanywa na serikali kupitia Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makaazi kwa kushirikiana na Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi).

Akizungumza jana na wadau wa miji, Ofisa Mipango Miji Mkuu kutoka Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makaazi, Tomi Kapinga, alisema kazi hiyo inafanywa na kampuni nne, mbili za nchini na mbili kutoka nje ya nchi.Kapinga alizitaja kampuni ambazo zinaendelea na mchakato kuwa ni Q- Consult Ltd na Afri - Arch Associates za nchini na Dodi Moss Ltd ya Italia na Happold Ltd ya Uingereza.


Alisema kwa sasa kampuni hizo kwa kushirikiana, zimeshakamilisha hatua ya pili ya kutengeneza dira ya mpango miji ili wadau waweze kuijadili.
Akifafanua mchakato wa pili ulivyo, Mhandisi Mkuu wa Kampuni ya Afri - Arch Associates, Dk. Camilius Lekule, alisema pamoja na wenzake dira yao imegawanyika katika maeneo mbalimbali ya kuangalia.

Dk. Lekule alitaja maeneo makuu yaliyoangaliwa katika dira hiyo kuwa ni pamoja na kuangalia matumizi ya ardhi, mji mkongwe utakavyojengwa na kuangalia namna miundombinu itakavyopita.

No comments:

Post a Comment