Pages

Friday, February 22, 2013

MIMI NA ADAM JUMA TUKO SAFI – TUNDAMAN

NYOTA wa muziki wa Kizazi Kipya ‘Bongo Fleva’, Tundaman amefurahi kumalizika kwa hali iliyokuwa ikimkosesha raha, ya mtayarishaji mahiri wa video, Adam Juma kumwekea kinyongo.
Kinyongo cha Adam Juma kwa Tunda, kilikuja baada ya nyota huyo kuamua kuirudia video ya kibao chake cha ‘Demu Sio’ nchini Kenya, kwa madai kuwa awali haikurekodiwa kiubunifu.
“Hivi sasa mimi na Adam tumerejea kuwa maswahiba kama ilivyokuwa mwanzo, baada ya kupuuzia lile lililotokea, kiukweli nafurahishwa sana na hali hiyo,” alisema Tunda katika maongezi yake na Saluti5.

No comments:

Post a Comment