Pages

Thursday, February 28, 2013

YANGA 1 – KAGERA 0


KIUNGO Mshambuliaji wa Yanga, Haruna Niyonzima, jana ameiwezesha timu yake kutimiza jumla ya Pointi 42, baada ya kuifungia bao pekee dhidi ya Kagera Sugar, katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara, uliopigwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Unaweza kusema chochote juu ya kiungo huyu wa kimataifa mzaliwa wa Rwanda, lakini ukweli utabaki pale pale kuwa kwasasa Niyonzima ndio roho ya Yanga. Ni aina ya mchezaji ambaye utampenda tu bila kujali itikadi yako.
Niyonzima aliipatia timu yake bao hilo katika dakika ya 65, baada ya kupokea pasi nzuri kutoka kwa Oscar Joshua, ambapo alimpunguza kiungo wa Kagera, George Kavila na kuachia shuti kali lililotinga katika engo ya nyuzi 90 na kumshinda kipa Hannington Kalyesubula, aliyebaki akiutazama tu mpira huo wakati ukitinga wavuni.
Kwa mara nyingine tena, Niyonzima aliwafundisha wachezaji wa Yanga namna ya kutumia nafasi zinazojitokeza kama alivyofanya katika mechi iliyopita dhidi ya Azam.
Washambuliaji wa Yanga walishindwa kutengeneza mazingira ya kutumbukiza mpira wavuni ikiwemo penalti walizozawadiwa mwishoni mwa kipindi cha kwanza na kupotezwa na Didier Kavumbagu.

Kiuongo Dumayo naye alionyesha uwezo wa kuachia mashuti ya nmbali ambapo shuti lake moja liligonga mwamba huku linguine likipanguliwa na kipa.

No comments:

Post a Comment