KAJALA YUPO HURU, WEMA AMLIPIA FAINI YA MILIONI 13
MSANII Wema Sepetu amemlipia faini ya shilingi milioni 13 msanii
mwenzake, Kajala Masanja, na kumfanya awe huru. Mapema leo,
Kajala
alihukumiwa kwenda jela miaka 5 au kulipa faini ya shilingi milioni 5.
Kajala alikuwa anakabiliwa na kesi ya kuuza nyumba iliyowekwa kizuizini
na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) baada ya mumewe,
Faraji Agustino kukumbwa na tuhuma za kutakatisha fedha haramu.
Faraji
yeye amehukumiwa kwenda jela miaka mitano au kulipa faini ya shilingi
milioni 213. Kwa sasa Kajala yupo nyumbani kwao maeneo ya Oysterbay
jijini Dar es Salaam pamoja na ndugu na jamaa.
No comments:
Post a Comment