Pages

Saturday, March 23, 2013

Mashabiki Simba wazichapa wakimpokea Rage

Mashabiki wa klabu ya Simba jana walizichapa wenyewe kwa wenyewe kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam wakati walipokuwa wakimsubiri Mwe-nyekiti wao, Ismail Aden Rage aliyekuwa akitokea nchini India kutibiwa.

Mashabiki hao wa Simba wal-izichapa baada ya kugundua baadhi yao walikwenda uwan-jani hapo kwa lengo la kum-fanyia vurugu mwenyekiti wao wakati wa mapokezi hayo.

Gazeti hili lilishuhudia mashabiki hao wa Simba walio-kaa kwa muda wa saa mbili uwanjani hapo kabla ya kuwasi-li kwa Rage na pia lilishuhudia mashabiki hao wakitwangana.

Kabla ya mashabiki hao kut-wangana, mashabiki waliokuwa wakimuunga mkono mwenyekiti wao walikuwa wakiimba nyimbo mbalimbali na walionekana wenye matumaini makubwa na Rage huku wakisisitiza bado wanautambua uongozi wake na hakuna anayeweza kumuondoa zaidi yao wenyewe.
Hata hivyo, baadaye lilitokea kundi dogo la mashabiki wa Simba ambalo lilisadikiwa kuwa ni kundi la Mpira Pesa ambalo limekwenda uwanjani hapo kwa ajili ya kufanya fujo na hivyo kuanza kushambuliwa kwa makonde wakidaiwa kuhusika na mkutano uliotangaza kum-wondoa Rage madarakani.

Mmoja wa mashabiki wa kla-bu hiyo ambaye alijitambulisha kwa jina la Shaban anayetokea tawi la makao makuu ya klabu ya Simba alisema bado Rage ataendelea kuwa Mwenyekiti na hawayatambui mapinduzi yali-yofanywa na baadhi ya watu wa Simba.

“Yale yalikuwa maneno ya watu, sisi hapa ndiyo Simba, bila sisi hakuna Simba, Rage ndiyo Mwenyekiti wetu na ataendelea kukaa madarakani mpaka sisi tutake wenyewe kumwondoa, wale Mpira Pesa walikuwa wan-ajisumbua na hapa hang’olewi mtu, hii ndiyo Simba bwana na sisi ndiyo wenye timu,” alisema Shaban huku wenzake wakimuunga mkono kwa kupiga mavuvuzela.
Mara baada ya Rage kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Julius Nyerere, alipitia mlango wa watu maalumu VIP na ali-potoka aliwasalimia mashabiki waliokuwa wakimshangilia na alikwenda moja kwa moja kati-ka gari aliloandaliwa huku aki-waambia waandishi wa habari wajionee wenyewe kama kuna mapinduzi yoyote yanayozung-umzwa juu yake.

“Awali ya yote namshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuende-lea kupigania afya yangu kwani kwa sasa ni ninaendelea vizuri, wingi wa watu hawa unatosha kunitambua mimi ni Mwenyeki-ti halali wa Simba na ninashan-gazwa kusikia kuna mapinduzi, hii ni ajabu sana,”alisema Rage.

Alisema,”Nyinyi wenyewe ni mashuhuda, angalieni hapa kuna mapinduzi kweli? wanao-taka mapinduzi ni watu wach-ache wanaotaka kuiharibu Sim-ba na kuleta migogoro isiyofaa?, sijiuzulu hata kidogo eti kwa kuwaogopa matapeli wachache, nitafanya hivyo endapo nitaona mimi mwenyewe napaswa kuji-uzulu, lakini siyo kwa kushini-kizwa.”

No comments:

Post a Comment