Pages

Wednesday, March 20, 2013

Mwanamke anusurika kupoteza maisha nchini India baada ya kuruka katika ghorofa la hoteli kupitia dirishani akiepuka shambulio la kutaka kubakwa.


Ghorofa la hoteli inayosadikiwa kutokea tukio hilo. 
Mwanamke mmoja raia wa Uingereza anaendelea kupata nafuu kufuatia majeraha aliyoyapata baada ya kuruka kupitia dirishani katika hoteli aliyokuwemo, kukimbia kile kilichoitwa shambulio la kutaka kubaka katika mji wa Agra nchini India.
Kwa mujibu wa Polisi, tukio hilo limetokea katika eneo la Cantonment mjini humo, katika majira ya alfajiri.

Naibu Supaintendent wa Polisi Simranjit Kaur amekaririwa akisema kuwa mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 31, aliruka kutoka katika dirisha la ghorofa ya pili baada ya mmiliki wa hoteli hiyo kujaribu kuingia chumbani kwake akidai kutaka kuchuliwa misuli (Massage).
Amesema mwanamke huyo aliingiwa na uoga wa kubakwa uliosababisha kuruka ghorofani humo.
Hata hivyo Kaur amesema polisi inamshikilia mmiliki wa hoteli hiyo na huenda wakafungia leseni ya biashara hiyo, kutokana na matokeo yatakayopatikana baada ya uchunguzi kukamilika.

No comments:

Post a Comment