Pages

Sunday, March 24, 2013

Rich Mavoko ndani ya usiku wa Rhyme Club Billz usiku huu

MKALI wa bongo fleva nchini, Rich Mavoko, leo anatarajiwa kufanya onesho kwenye ukumbi wa kimataifa wa Club Bilicanas uliopo katikati ya Jiji la Dar es Salaam.

Onesho hilo lililobatizwa kama ‘Usiku wa Rhyme’ linatarajiwa kuwa la aina yake, hasa ikizingatiwa ni msanii anayejua nini wapenzi na mashabiki wake wanataka kukiona jukwaani.

Akizungumzia onesho hilo, Mavoko alisema si la kukosa kwani amepania kuwapa vitu adimu mashabiki wake, hivyo amewaomba kujitokeza kwa wingi.
Alisema anatarajia kuwapa utamu zaidi kupitia vibao vyake kuanzia vya zamani hadi kile kipya alichokiachia hivi karibuni kiitwacho, One Time.

“Nawaomba mashabiki kujitokeza kwa wingi katika onesho langu la Jumapili kwani nimewaandalia mambo makubwa ambayo yataweka historia,” alisema.
Mbali na wimbo huo mpya, Mavoko amepata kutoka na singo kadhaa ambazo ziliweza kufanya vema katika medani ya muziki nchini zikiwemo ‘Silali’, ‘Mary Me’, ‘Uzuri Wako’, ‘Follow Follow’, ‘Bolingo Nangai’ na nyinginezo.

No comments:

Post a Comment