Pages

Wednesday, March 20, 2013

Tatu zashuka daraja la kwanza Tanzania

WAKATI Ligi Daraja la Kwanza (FDL), ikimalizika mwishoni mwa wiki iliyopita, imeshuhudiwa timu za Small Kids ya Rukwa, Moro United ya Dar es Salaam na Morani Fc ya Manyara zikishuka daraja hadi Ligi ya Mkoa msimu ujao.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, jana, Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Boniface Wambura, alisema Moro United imeaga ligi hiyo kutoka Kundi B, huku Kundi C ikiaga Morani.

Alisema Small Kids iliyokuwa Kundi A, imeshuka baada ya kuondolewa kwenye michuano hiyo mapema, kwa kushindwa kufika uwanjani kwenye moja ya mechi zake.
Wambura alizitaja timu zilizopanda Ligi Kuu ya Vodacom msimu wa 2013/2014 ni Mbeya City ya Mbeya iliyoongoza kundi A, Ashanti United ya Dar es Salaam Kundi B na maafande wa Rhino Rangers ya Tabora kutoka Kundi C.

No comments:

Post a Comment